JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anwani ya simu: “MAKAMU” Mji
wa Serikali
Simu Na.: +255 26 2329006 Eneo
la Mtumba,
Fax Na:+255 26 2329007 Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais.
Barua Pepe: km@vpo.go.tz Ihumwa,
S.L.P 2502
DODOMA
TANZANIA
Dodoma, Novemba 04, 2019
TAARIFA
KWA UMMA
Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea
kusimamia marufuku ya katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kushirikiana
na Kikosi kazi cha Kitaifa. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la uzalishaji,
utengezaji na uingizaji na usambazaji wa mifuko isiyokidhi viwango vilivyowekwa
na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Kikosi kazi cha Kitaifa cha
kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki pamoja na Kamati za Mikoa na Wilaya wanaendesha
oparesheni maalumu nchi nzima kwa lengo la kusaka mifuko isiyokidhi viwango.
Tarehe 30/10/2019 NEMC ilikamata
marobota 21 katika Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera na marobota 7 Mkoani Arusha
ambayo yanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Arusha. Upelelezi wa mashauri
haya bado unaendelea.
Leo tarehe 4/11/2019 Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi kwa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza wamekamata shehena ya mifuko
isiyokidhi viwango gunia 8 yenye thamani ya Shilingi 10,000,000/- Mifuko hiyo iliingia kupitia bandari bubu ya
Bwiru jijini Mwanza ikitokea nchi jirani. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani na
mifuko hiyo itateketezwa kwa mujibu wa sheria kama itakavyoelekezwa na NEMC.
Ofisi ya Makamu wa Rais,
inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na
uuzaji wa mifuko mbadala kuhakikisha wanazingatia matakwa ya Sheria. Aidha, wafanyabiashara
wanasisitizwa kuacha kuzalisha, kuingiza nchini, kuuza na kusambaza mifuko
isiyokidhi viwango. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote
wanaokiuka agizo hilo.
Imetolewa na
Lulu Mussa
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
No comments:
Post a Comment