Na Mwandishi Wetu.
Serikali ya Awamu ya Tano imeuwezesha mkoa wa Mbeya
kujenga miundombinu ya kisasa katika sekta zinazochangia kuleta ustawi kwa
wananchi ikiwemo afya.
Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila amesema kuwa mkoa huo umepiga hatua kubwa
katika kuleta mageuzi kupitia miundombinu iliyojengwa katika sekta za afya,
elimu, maji, uchukuzi na kilimo.
“Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 4 kwa
ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika mkoa wetu na ziko katika hatua za
mwisho kukamilika ili ziweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni
utekelezaji wa azma ya Serikali kuboresha sekta hiyo” Alisisitiza Chalamila
Akifafanua, mhe. Chalamila amesema kuwa mkoa huo
umefakiwa katika ujenzi wa Vituo vya Afya hali inayoboresha huduma zinazotolewa
katika sekta hiyo katika Halmashauri za Wilaya mkoani huo.
Sehemu ya Halmashauri za Wilaya zilizonufaika na
ujenzi wa Hospitali za Wilaya ni; Rungwe,Busokelo na Kyela,pamoja na upanuzi na ujenzi wa Vituo
vya Afya ili kutimiza lengo la Serikali kutoa huduma bora za afya kwa wananchi
wote.
Katika sekta ya Elimu Mhe. Chalamila amesema kuwa
Shilingi Bilioni 18 zimetolewa katika kuboresha sekta hiyo hivyo kukuza kiwango
cha elimu na ubora kutokana na uwekezaji huo uliofanywa na Serikali.
“Tumejipanga katika kukuza sekta ya viwanda na
tumetenga eneo maalum la uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na tayari baadhi ya wajasiriamali
wa mkoa huo wamepata fursa ya kwenda nchini China kujifunza namna ya kuanzisha
na kuendeleza viwanda vya usindikaji mbogamboga na matunda,” Aliongeza Chalamila
Akieleza zaidi, amesema kuwa mkoa huo umeweka mkazo
katika kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na uwekezaji unaofanywa na
Serikali katika sekta mbalimbali ili kuboresha hali ya maisha.
Aidha, Katika Halmashuri ya Wilaya ya Busokelo,
Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo
utakaogharimu shilingi Bilioni 5.3 ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa
wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri
ya Wilaya ya Rungwe Bi Rehema Peter amesema kuwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa
maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 5 utawanufaisha wananchi zaidi ya elfu
ishirini.
“Kukamilika kwa mradi huu wa maji kutaongeza
wananchi wanaofikiwa na huduma ya maji kutoka asilimia 65 hapo awali hadi kufikia
asilimia 80 hali itakayochochea kukua kwa shughuli za kiuchumi na ustawi wa
wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. James Kasusura
amesema kuwa wamefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo katika robo ya kwanza ya
mwaka 2019/2020 kwa kukusanya shilingi Bilioni 3.1 sawa na zaidi ya asilimia 26
ya lengo walilojiwekea.
Tumeweza kukarabati nyumba 25 za walimu katika Jiji
letu na pia tumejenga kituo cha afya Nzowe kwa shilingi milioni 700
zilizotolewa na Serikali.
Kipindi cha TUNATEKELEZA kinaratibiwa na Idara ya
Habari MAELEZO na kurushwa na Shrika la Utangazaji Tanzania, Awamu hii
ikiwashirikisha Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment