Habari za Punde

Waziri wa Afya afanya mazungumzo na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto UNICEF

 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto UNICEF Maha Damaj alipofika Ofisini kwake Mnazi mmoja Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo yake na  Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto UNICEF Maha Damaj alipofika Ofisini kwake Mnazi mmoja Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar    
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashidi Mohamed ameliomba Shirika la kuhudumia watoto Duniani UNICEF kufanya utafiti juu ya hali ya utapiamlo kwa watoto ambao wanakumbwa na tatizo hapa nchini
 Hayo ameyasema leo huko Ofisini kwake  wakati akizungumza na Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kanda ya Zanzibar Maha Damaj, amesema Zanzibar imekuwa na uzalishaji mkubwa wa chakula, matunda na mboga mboga lakini bado kumekuwa na ongezeko la tatizo hilo nchini.
Amesema tatizo la utapiamlo huwaathari watoto wengi kutokana na kukosa vyakula vyenye afya ambalo limeonekana katika vituo vya afya na skuli.
Amesema ipo haja ya kufanya utafiti ili kujua njia ya kuondosha tatizo hilo pamoja na kuelimisha jamii juu ya madhara  na kuwakinga watoto na madhara hayo.
“Watoto ndio taifa la kesho hivyo ipo haja yakuona wanakuwa vizuri  kwa kupata  vijana wenye afya na kulitumikia taifa lao badae”, alieleza Waziri Hamad
Waziri Hamad amesema maeneo yaliyoathirika zaidi na tatizo hilo ni Wilaya Micheweni kwa upnde wa Pemba na Mkoa wa Kaskazini Unguja ni maeneo ambayo yameonekana kutokea kwa vifo vingi vya kinamama na watoto.
Nae Mwakilishi Mkazi Bi Maha Damaj  Shirika lake litalishughulikia suala na kufanya utafiti na  kuhakikisha kwamba wanalipatia ufumbuzi na kujua sababu ya tatizo hilo katika maeneo hayo.
Aidha amesema kuwa yupo tayari kuitangaza Zanzibar na kuifanya kuwa ni kituo cha elimu ya malaria kutokana na mafanikio makubwa ya kutokomeza maradhi hayo kwa asilimia 0.2 jambo ambalo ni faraja kubwa duniani.
Hata hivyo Muwakilishi huyo amesema kuwa shirika lake litatoa vifaa vya kina mama na watoto katika vituo vya afya 36 vya Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.