Habari za Punde

Ufungaji wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kiswahili Lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akifunga Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Na Mwashungi Tahir      Maelezo     20-12-2019.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha lugha ya Kiswahili inazidi kuimarika siku hadi siku  kwa vizazi vya sasa na vijavyo ili viweze kufaidika.
Hayo ameyasema Waziri wa Nchi  Afisa wa Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais  Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ufungaji wa kongamano la Tatu la  Kiswahili la Kimataifa lililofanyika huko katika Ukumbi wa Sheikh  Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni .
Amesema lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inahitaji kukuzwa zaidi kwa wageni na wenyeji ili iweze kuwa mstari wa mbele katika kuzungumzwa ndani na nje ya nchi.
Aidha amesema lugha ya  Kiswahili haistahiki kubezwa kwani ni lugha inayothaminiwa na kuitaka jamii kuiendeleza na kuipa hadhi yake ya lugha hiyo   kama lugha nyengine.
Hivyo alisema ni wajibu wetu  kuithamini lugha ya Kiswahili na kuitumia katika matumizi sahihi kwani sie waswahili ni  lazima kujivunia lugha yetu na sio nyengine bali ni Kiswahili.
Pia amesema Nchi nyingi duniani zinatumia lugha ya Kiswahili  kufundishia katika vyuo vikuu  na sehemu mbali mbali hasa ikiwemo Nchi ya Italia
Vile vile aliwataka waandishi chipukizi kutumia lugha ya Kiswahili ya ufasaha yenye kueleweka na kuwaiga waandishi wakongwe kama Shafi Adam Shafi ili kuiga kipaji chake na wao waweze kuendeleza mbele vipaji vyao.
Pia Balozi Seif alisema kuwa fursa ya Kiswahili ni hazina ya uchumi kujiongeza na kukidhi mahitaji maalum ya kibinaadamu  na kuwataka jamii kuacha kuiga lugha za wenzetu.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili BAKIZA Amina AliKhamis  akitoa maazimio ya Kongamano la tatu  la Kiswahili amesema,Rais awe na mshauri wa masuala ya lugha, kujenga mshikamano zaidi kwa taasisi zinazounda istilahi na msamiati na wanahabari wa Kiswahili wawe wataalamu wa Kiswahili.
Kwa upande wa wageni walioshiriki kongamano hilo wamesema wamefaidika na mada zilizotolewa hapo na kuahidi watayafanyia kazi.
Aidha katika washiriki hao walipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali  za historia, bandarini, miti ulaya na kwahaji Tumbo ikiwa  na lengo lake kuona sehemu alozitumia mwandishi mkongwe Shafi Adam Shafi.
Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Ali Abeid  Karume akizungumza katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Picha ya pamoja wakiwemo viongozi mbalimbali na Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Kiswahili wakiwa katika ziara huko Bandarini Mjini Zanzibar.
PICHA NA MARYAM KIDIKO - MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.