Habari za Punde

Mbwana Ally Samatta Aanza Mazoezi Rasmin Timu Yake Mpya ya Aston Villa.


Samatta aliyesajiliwa Aston Villa wiki hii kwa dau la Pauni Milioni 10 kutoka KRC Genk ya Ubelgiji anatarajiwa kuanza kazi rasmi katika klabu yake hiyo mpya Jumanne itakapomenyana na Leicester City katika Kombe la Ligi England  

Na Bakari Madjeshi. Michuzi TV

Mshambuliaji mpya wa Aston Villa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Ally Samatta rasmi ameanza mazoezi na Klabu yake hiyo ya nchini Uingereza baada yakukamilisha usajili wake wa ada uhamisho ya £10m akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.

Samatta aliyekuwa na ndoto zakucheza soka nchini Uingereza huenda akaanza kuichezea Aston Villa mchezo wake wa kwanza katika mchezo wa Nusu Fainali ya mkondo wa pili, Michuano ya Carabao Cup dhidi ya Leicester City ya nchini humo, Januari 28, 2020.

Samatta aliyesajiliwa Aston Villa kuziba pengo la Mshambuliaji, Wesley aliyeumia klabuni hapo atakuwa na kazi nyingine yakuhakikisha pengo la Mshambuliaji huyo linazibwa ipasavyo katika kikosi hicho, kazi hiyo huenda ikaanza katika mchezo wa Januari 28 dhidi Leicester baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya bao 1-1.

Samatta amefanya vizuri akiwa na Kikosi cha KRC Genk ya Ubelgiji hadi kuzifunga Klabu maarufu na kongwe barani Ulaya, timu za Liverpool katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu wa 2019-2020.

Nahodha huyo wa Tanzania huenda akawa mfano tosha kwa Wanandika wa nchini humo kuiga mfano wake sambamba na jitihada zake binafsi nakupeperusha bendera ya taifa la Tanzania katika medani ya soka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.