Habari za Punde

Ujumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Watembelea NEC

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiRufaa (Mst) Semistocles Kaijage (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) Jaji Dkt. Jane Ansah ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage akifungua kikao baina ya Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) na NEC Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk na kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) Jaji Dkt. Jane Ansah. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage (kulia) akimkabidhi zawadi ya saa yenye nembo ya NEC, kiongozi wa Ujumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, JajiDkt. Jane Ansah.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Sekretarieti wakifurahia jambo kwa kupiga makofi wakati wa majadiliano baina ya NEC na Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo. 
Viongozi wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Malawi (MEC) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Tume hizo na maafisa waandamizi leo Jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya MEC na NEC.
 Picha na Idaraya Habari na Elimu ya Mpiga Kura-NEC

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.