Habari za Punde

Uzinduzi wa Skuli Mpya ya Sekondari Rahaleo Zanzibar Kwa Niaba ya Skuli Tisa za Unguja na Pemba Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria Ufunguzi wa  jengo la Skuli ya Sekondari ya Rahaleo kwa niaba ya Skuli Tisa za Unguja na Pemba, ikiwa ni shamrashamra za Kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Rahaleo Jijini Zanzibar.(kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Mhe.Riziki Pembe Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa  jengo la Skuli ya Sekondari ya Rahaleo kwa niaba ya Skuli Tisa za Unguja na Pemba, ikiwa ni shamrashamra za Kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Rahaleo Jijini Zanzibar.(kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Mhe.Riziki Pembe Juma. na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zuberi Ali Maulid.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mwalimu wa Somo la Sayansi Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.Ndg. Issa Masoud, alipotembelea maabara ya Sayansi katika skuli hiyo (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Riziki Pembe Juma.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mwalimu wa Somo la Sayansi Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.Ndg. Issa Masoud, alipotembelea maabara ya Sayansi katika skuli hiyo (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Riziki Pembe Juma.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Bi.Asia Iddi Issa  akitowa maelezo ya kwa Rais wakati alipotembelea darasa la Komputa katika Skuli hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi uliofanyika katika jengo hilo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Eng.Dkt.Idrisa Muslim Hija akitowa maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi wa Skuli Tisa za Sekondari zilizojengwa Unguja na Pemba, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Rahaleo Jijini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wa Uhamasishaji wakishangilia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Rahaleo kwa niaba ya Skuli Tisa za Sekondari zilizojengwa katika maeneo ya Unguja na Pemba, wakati wa hafla ya ufunguzi huo ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli Tisa za Sekondari zilizojengwa Unguja na Pemba wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Rahaleo Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.