Habari za Punde

BONGOZOZO: Kunyweni Maziwa ya ASAS Yana Ubora wa Kimataifa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri akiwa na balozi Maziwa ya AsasNick Reynolds 'Bongo Zozo' wakizungumza na wandishi wa habari mkoani Iringa,mara baada ya kumtangaza rasmi Bongozozo kuwa balozi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri akiwa na balozi Maziwa ya AsasNick Reynolds 'Bongo Zozo' wakizungumza na wandishi wa habari mkoani Iringa,mara baada ya kumtangaza rasmi Bongozozo kuwa balozi wa kampuni hiyo.

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
BALOZI wa kampuni ya Maziwa ya Asas amewataka watanzania kunywa maziwa bora yanayozalishwa na kampuni ya maziwa ya Asas iliyopo mkoani Iringa kwakuwa wamekidhi vigezo vyote ya kimataifa.

Akizungumza na vyombo vya habari Nick Reynolds 'Bongo Zozo' alisema kuwa watanzania wanatakiwa kutumia maziwa bora ambayo yanatengenezwa hapa nchini hasa na kampuni hii ya Asas hasa kwa wale wanamichezo hivyo hata akiwa viwanjani ataendelea kuitangaza bidhaa ya asas kutokana na ubora wake.

SHABIKI aliyejizoelea umaarufu wa soka nchini hivi karibuni, Nick Reynolds 'Bongo Zozo' anatarajia kuwaongoza maelfu wa mashabiki mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo kati ya Lipuli na Simba na kuwataka mashabiki wa soka mkoani Iringa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu ya Lipuli Fc’ Wanapaluhengo katika mchezo wake dhidi ya Simba unaochezwa leo katika dimba la Samora

 “Nitakuwa uwanjani nakunywa maziwa ya Asas huku nikihamasisha mashabiki kunywa maziwa ya Asas na kuipenda timu yao ya nyumbani kama Lipuli hivyo nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwenye mchezo wa simba na Lipuli” alisema bongozozo

Alisema kuwa amekaa Iringa miaka 13 hali inayomfanya kuipenda zaidi Lipuli Fc timu ambao imekuwa ikifanya vyema dhidi ya vigogo hao na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Samora leo kwani atakuwepo uwanjani.

Alisema mashabiki watakaojitokeza siku ya leo atahakikisha anatoa zawadi ya jezi za Lipuli na atakaa jukwaa la mashabiki wa kawaida kufanya fujo isiyoumiza kama ilivyoada ya kushangilia timu ya Taifa kila inaposhiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Nimekuja Iringa kuhakikisha tunashangilia wanapaluhengo hivyo tujitokeze kwa wingi leo katika mechi yetu dhidi ya Simba tuweze kuibuka na ushindi na mashabiki waje kushuhudia fujo zisizoumiza ambapo nitakaa kwenye jukwaa la mashabiki wa kawaida na kugawa jezi” alisema

Bongozozo ambaye amekuja katika mchezo huo kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya Asas aliwataka mashabiki kutumia maziwa ya Asas pindi wanaposhangilia kwani wanapata nguvu za kushangilia bila kuchoka kutokana na ubora wa maziwa hayo nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri alisema kuwa kampuni ya Asas imeamua kufanya kazi na Bongozozo kwa kuwa amekuwa mmoja wa mabalozi wazuri wa soka nchini hivyo wanajisikia faraja kufanya kazi naye kwani atasaidia kutangaza bidhaa zao za maziwa ndani na nje ya nchi.

“Huyu ni balozi wetu mpya wa bidhaa za maziwa ya ASAS. Na huu ni sehemu ya mkakati wetu wa kuwahamasisha watanzania kunywa maziwa kwa wingi kwani kila mtu anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka hivyo Bongo zozo atasaidia sana katika kampeni hii” alisema. 

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) mtu mmoja anatakiwa kunywa wastani wa lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini takwimu za hapa nchini zinaonesha unywaji wa maziwa hayo upo chini ya asilimia 40 hali inayolazimu kuwatumia watu maarufu kuhamasisha watu wanywe maziwa zaidi hasa kutoka kampuni ya Asas. 

Alisema kuwa kwa upande wa kampuni hiyo mstari wa mbele katika kudhamini michezo mbalimbali inayofanyika ndani ya Iringa na nje ya Iringa ikiwemo kuidhamini timu ya Lipuli na ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa ambapo wamedhamini kwa miaka 3.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.