Habari za Punde

Majaliwa Kufungua Mkutano wa Mawaziri SADC kwa Njia ya Video


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.

Na Erick Msuya- MAELEZO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua kikao cha Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha Uchumi pamoja na viwanda na Biashara utakaofanyika Jijini Dar es Salaam 16, Machi kwa njia ya Video kufuatia tishio la virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert Ibuge katika kituo cha mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) baada ya kutoa taarifa fupi ya kikao cha dharura cha Mawaziri wa SADC sekta ya Afya kilichojadili hali halisi ya Ugonjwa wa Corona  (CODIV- 19)  katika Nchi za SADC.

Amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na kuendeshwa kwa njia ya mfumo wa Video (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.

“Kufatia Ushauri uliotolewa katika maazimio ya kikao cha Mawaziri wa Afya wa SADC, kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC sasa hivi kitafanyika kwa njia ya video  tofauti na ilivyozoeleka, hivyo kila Nchi mwanachama wa SADC atakuwa nchini kwake huku wakijadili kwa njia ya video” alisema Balozi Ibuge.

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mtendaji wa Maswala ya Ushirikiano wa Kikanda (SADC) Thembinkosi Mhlongo amesema kuna haja ya Nchi wanachamawa SADC kutumia hati ya kusafiria (Pasport) inayoweza kumruhusu kila Mwanachama kusafiri na kufanya Shughuli za maendeleo katika umoja ya Nchi Wanachama wa SADC bila bugudha.

“Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine ziweza kutumia Hati zao za kusafiria, na sisi tunahaja ya kuwa na hati zetu za kusafiria tukiwa kama SADC, katika jumuiya yetu kuna watu watafanya kazi kwa muingiliano wa kikanda hivyo ni muhimu kutumia hati moja” Alisema Mhlongo.

Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni mazingira uwezeshiji wa maendeleo ya viwanda, masuala ya fedha na Michango ya Jumuiya, hati za kusafiria za SADC, na uanzishwaji wa shirika la utalii kwa nchi za kusini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.