Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli Apokea Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Kwa Mwaka 2018/19 Pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa PCCB Katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripotiya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma Muhtasari wa Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka 2018-2019 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/19, moja kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akisoma Muhtasari wa Taarifa yake ya Mwaka 2018-2019 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Taarifa ya Mwaka 2018/2019 ya CAG pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi mara baada ya kuwakabidhi pamoja na Taarifa ya TAKUKURU kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alipokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/2019 kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu, pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakitoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.