Habari za Punde

TFS SAO HILL:WADAU TUSAIDIE WATOTO YATIMA

Afisa Utumishi wa Shamba la Miti Sao Hill Felista Bayo akikabidhi msaada huo kwa msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha SISI NI KESHO 
Picha ya watoto yatima na wafanyakazi wa kituo cha watoto yatima cha SISI NI KESHO wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Sao Hill Mufindi

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
Wadau mbalimbali wametakiwa kuendelea kuwachangia na kuwakumbuka Watoto wenye mahitaji maalumu na yatima kwa lengo la kuwafariji kwa kuwasaidia kupata mahitaji yao muhimu kama ambavyo familia nyingine zinapata majumbani yao.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wanawake wa Shamba la Miti Sao Hill,Afisa Utumishi wa Shamba la Miti Sao Hill Felista Bayo alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa na moyo wa kujitolea kusaidia Watoto ambao hawana uwezo na wale yatima ili nao watimize malengo yao.

Alisema kuwa Baadhi ya watumishi wanawake kutoka TFS - Shamba la Miti Sao Hill wamekuwa wakijitolea kusaidia Watoto yatima mara kwa mara kwa lengo la kuifanya jamii nyingine kuiga mfano huo wa kusaidia Watoto.

Bayo alisema kuwa Vifaa walivyokabidhiwa ni sukari, mchele mafuta ya kupikia na kupaka, sabuni , pampers, kandambili, chumvi, track suit, sweta, juice, biscuits, blanketi, unga wa lishe na mahindi kwa kuwa hayo ndio mahitaji ya Watoto hao.

“Tulitembelea kwanza kituo hicho na kujua mahitaji ambayo yanahitajika na kuyatafuta ndio maana tulipeleka mahitaji hayo kulingana na mahitaji ya kitu cha Watoto yatima cha SISI NI Kesho kilichopo katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi katika Mkoa wa Iringa” Bayo

Bayo alisema kuwa vifaa vinavyokabidhiwa vina thamani ya shilingi laki sita sitini na moja elfu (Tsh 661,000/=) ambapo fedha hiyo imechangwa na wanawake wafanyakazi wa shamba la miti ya Sao Hill

Naye Msimamizi wa kituo hiko Bi. Jane Mkondola ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuchangia kituo hiki na watu wengine wenye mahitaji ili kuwezesha malezi ya watoto kuwa mazuri zaidi kwani lengo la kituo hiki sio kujipatia faida bali ni kutoa huduma.

Watumishi wanawake TFS - Shamba la Miti Sao Hill wamekuwa wakisaidia vituo vya watoto yatima Kila mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.