Habari za Punde

Virusi vya Corona: Jimbo la Missouri laipeleka China mahakamani

GETTY IMAGES
Image captionRais wa China Xi Jinping akiwa na Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus. Rais wa Marekani Trump 'ameilaumu' WHO kupendelea Chinda.
Na.BBC.
Missouri limekuwa jimbo la kwanza nchini Marekani kuishitaki serikali ya Uchina kwa namna ambayo imeshughulikia janga la virusi vya corona.
Mashtaka hayo yanakuja wakati ambao kuna ongezeko la matukio ndani ya Marekani kuinyooshea vidole vya lawama China kuhusu janga la corona.
Rais Donald Trump mwanzoni aliisifu China kwa namna ilivyoshughulikia janga la virusi vya corona, lakini baada ya kuwa kwenye shinikizo kubwa kuhusu mlipuko huo, aliituhumu China kuwa ndio chanzo.
Hivi karibuni ametangaza kusitisha msaada wa kifedha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) akilishutumu kuvutia upande wa China katika janga hili.
Wakati uchaguzi wa Marekani ukitarajiwa mwaka huu, waangalizi wanasema kuwa mashtaka ya Missouri-sambamba na mashtaka mengine ya makampuni nchini Marekani -huenda ukawa mwisho wa kisiasa wa chama cha Trump cha Republican.
''Tunaona watu wengi wanatumia suala la China kufunika makosa ya serikali ya Marekani,'' Tom Ginsburg, profesa wa masomo ya sharia za kimataifa katika chuo kikuu cha Chicago aliiambia Reuters.
China yenyewe haitakuwa na jambo la kuogopa kuhusu mashtaka hayo. Serikali za kigeni zinalindwa dhidi ya kushtakiwa katika mahakama za Marekani na kama Marekani ilitaka kuishutumu China, ingefanya hivyo kwenye majukwaa ya kimataifa ambapo Beijing ingekuwa na haki ya kujibu.
Virusi vya corona vilipuka jijini Wuhan, China mwishoni mwa mwaka jana. Kufikia sasa Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi duniani 826,240.
Jimbo la Missouri linaishtaki serikali ya China kwa namna walivyoshughulikia janga la corona jambo lililosababisha athari kubwa za kiuchumi
Katika mashtaka hayo, mwanasheria Mkuu wa jimbo la Missouri Eric Schmitt ameituhumu China kuwa haikufanya jitihada za kutosha kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
Bwana Schmitt amedai kuwa wakazi wa jimbo la Missouri wameathirika baada ya kupata hasara ya kiuchumi ya thamani ya mabilioni ya dola .
Lakini wataalamu wa masuala ya sharia wana mashaka kuhusu namna jimbo hilo litakavyokwenda na mchakato wa hatua hizo za kisheria na msukumo zaidi kuhusu mchakato huo.
Mwanasheria mkuu amesema kwenye jimbo la Missouri athari za corona ni kubwa sana.
"Familia zimetengana na wapendwa wao waliofariki kutokana na corona," amesema Schmitt.
''Hali ya kiuchumi ya wafanyabiashara wadogo ni mbaya na wengi wameanza kufunga biashara zao, na wale wanaoishi kwa ujira wa siku wanapata tabu kutimiza mahitaji yao ya chakula kila siku.''
Mpaka sasa jimbo hilo limethibitisha kuwa na wagonjwa 5,941 na vifo 189.
"Serikali ya China iliudanganya ulimwengu kuhusu hatari ya virusi vya Covid-19, ikanyawanyamazisha watu waliotoa taarifa kuhusu janga hili kwa mara ya kwanza na haikufanya jitihada za kuzuia kuenea kwa ugonjwa''.
Schmitt ametaka China iwajibike kwa vitendo vyake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.