Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Akabidhi Gari 50 za Kubebea Wagonjwa Kwa Wabunge.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na baadhi ya wabunge waliokabidhiwa  funguo  za magari ya kubebea wagonjwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 29, 2020. Magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi bilioni 6 yalikabidhiwa kwa wabunge.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea shukurani kutoka kwa Mbunge wa Mbulu Vijijini Fratei Massay wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kulia) wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya   shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) wakifurahia wakati  Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (kulia) alikionyesha ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhiwa wakati Waziri Mkuu alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Amina  Makilagi wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya   shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya   shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandishi, Stella Manyanya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tatu kulia ni Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi, Stella Manyanya.
Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya akitazama gari la kubebea wagonjwa la Kituo cha Afya cha Mbamba Bay wakati Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya   shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. 
Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellla Manyanya akilala chini ikiwa ni ishara ya shukurani na furaha iliyokithiri kwa mujibu wa mila za wangoni na wamatengo wakati alipokabidhiwa ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
                                                        
                                                              (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.