Habari za Punde

Rais Dk Shein atuma salamu za rambi rambi kwa Rais Dkt Magufuli kufuatia kifo cha Balozi Mahiga


STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                 03.05.2020
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kufuatia kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria  Balozi Augustine Mahiga.

Balozi Mahiga alifariki nyumbani wake Mjini Dodoma baada ya kuugua hafla ambapo alipofikishwa hospitali tayari alikwishapoteza uhai na kuzikwa jana Mkoani Iringa.

Katika salamu hizo Dk. Shein alisema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Agustine Mahiga kilichotokea Mjini Dodoma.

“Kwa niaba ya watu wa Zanzibar na Serikali natoa mkono wa pole na rambirambi kwako Mheshimiwa Rais, familia ya marehemu pamoja na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msiba wa kuondokewa na kiongozi aliyekuwa na upendo wa nchi yetu”, ilieleza sehemu ya salamu hizo za rambirambi alizozituba Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alisema  Balozi Mahiga ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi katika shughuli za kimataifa ikiwemo Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na taasisi nyengine.

Dk. Shein alisema kuwa Balozi Mahiga alikuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na kudumisha umoja, amani na upendo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata misingi ya Katiba na Sheria.

Rais Dk. Shein alimuomba Mwenyezi Mungu awajaalie wafiwa na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania moyo wa subira katika kipindi hichi cha msiba.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.