Habari za Punde

Watanzania Watakiwa Kutumia Mitandao ya Kijamii Kwa Faida.

Muongozaji wa majadiliano Bw. Michael Gwimile akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Habari ulioandaliwa na MISA-Tan na kufanyika hivi karibuni Jijini Dodoma.
Muongozaji wa majadiliano Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bw. Athumani Mtasha  akifafanua kuhusu nafasi ya polisi katika kudhibiti makosa ya kimtandao na ushirikiano na vyombo vya Habari wakati wa mkutano wa majadiliano ulioandaliwa na MISA-Tan na kufanyika jijini Dodoma.
Washiriki wa mkutano wa majadiliano wakiwa wamekaa kwa kuzingatia umbali wa mita moja wakifatilia majadiliano wakati wa mkutano wa wadau kuhusu changamoto za matumizi sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

NA FREDY MGUNDA,DODOMA.
WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa za uhakika katika mitandao ya kijamii ili kuondoa upotoshaji ambao umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kuzua taaruki kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania  (MISA -TAN) iliyowakutanisha wadau  mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii, Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman Mtasha alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa za mamlaka mbalimbali zisizo wahusu bila uchunguzi matokeo yake husababisha uchochezi ,takwimu za uongo na kusababisha taharuki katika jamii hivyo ni vyema watu wakaacha mara moja tabia ya kusambaza taarifa kwani zinaweza kuwatia hatiani.

Alisema kuwa Kwa mujibu wa takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kumekuwa na ongezeko kubwa la Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania na ongezeko hilo limepanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa miongoni mwa Wananchi na Taasisi mbalimbali. 
Mtasha alisema kuwa mitandao ya kijamii hususani facebook, twitter, Instagram na youtube imewawezesha wananchi kuzalisha, kusambaza na kupata taarifa mbalimbali za matukio yanayojiri katika jamii kwa haraka Zaidi  kuliko redio, televisheni na magazeti.
“Pamoja na fursa hii kumekuwa na changamoto ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii zikiwemo upotoshaji, udhalilishaji na matumizi mengine yasiyofaa na Hii inajidhihirisha kwenye kuongezeka kwa kesi za makosa ya kimtandao katika miezi ya hivi karibuni” alisema

Afisa sheria Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]Kanda ya kati Joseph Kavishe amesema mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine likiwemo Jeshi la polisi  imeendelea kusimamia kwa ueledi vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao .
“TCRA imeendelea kusimamia kwa ukaribu sana vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao, kwa Maagizo ya Mhe.Rais kuhusu taarifa za Uzushi yeyote anayekamatwa lazima taraibu za kisheria kufuatwa,TCRA inasimamia vyombo vya Habari kwa mashauriano pengine panapokuwa na changamoto Fulani ya utoaji wa Habari  huwa kuna kamati ya maudhui na si kila kosa lazima kuadhibiwa na makosa mengine kamati ya maudhui hukaa na kuwaonya wahusika ili kuacha kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Mjumbe wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Michael John Gumile ambaye pia ni Mhadhili kutoka chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St.John) alisema Warsha hiyo ya wanahabari imesaidia wadau wa Habari namna ya kuandika Habari zitakazosaidia kuondoa taharuki katika jamii hususan katika kipindi hiki cha Corona.
Sasa hivi nchini na Dunia kwa ujumla hivyo wadau wa Habari tumekutana hapa katika kujenga msingi mzuri ili kuhakikisha taarifa sahihi zinapatikana na watu kuzifanyia maamuzi na taarifa ambazo haziwezi kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Meneja wa kituo cha Redio,Dodoma FM ,Zania Miraji ni miongoni mwa wadau wa Habari waliohudhuria katika warsha  hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika ,hapa nchini(MISA-TAN) alisema warsha hiyo imekuwa mwarobaini wa kuwakumbusha waliojifunza kutoka vyuoni na na maelekezo yaliyotolewa katika warsha hiyo watayafanyia kazi hususan namna ya kuandika Habari ambazo hazina mkanganyiko pia namna ya mwanahabari ya kujikinga

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.