Habari za Punde

Breaking News Mwanamke wa Pili Kada wa CCM Ajitokeza Kuchukua Fomu ya Urais Mhe. Hasna Attai Masoud Akiwa Mhgombea wa 25 Kijitokeza Kuchukua Fomu ya Urais wa Zanzibar Kutia CCM.

Kada wa 25 wa Chama cha Mapinduzi Akiwa Mwanamke wa Pili kujitokeza katika Kinyanganyiro cha kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe.Hasna Attai Masoud akitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar akiwa na Wapambe wake wakimshindikiza kuelekea katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, baada ya kukamilisha zoezi hilo la uchukuaji wa Fomu leo 24-6-2020.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi akiwa Mgombe wa Pili Mwanamke Mhe. Hasna Attai Masoud akiwa na mkoba ukiwa na famu zake za kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg Galos Nyimbo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar. 
Katibu Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Mkoba ukiwa na Fomu za kuwania kinyanganyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe. Hasna Attai Masoud, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kiswandui Jijini Zanzibar.
Katibu Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu za kuwania kinyanganyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe. Hasna Attai Masoud, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kiswandui Jijini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM wa 25  Mhe. Hasna Attai Masoud akijaza namba za Kadi yake ya CCM katika daftari ya kuchukua Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, akiwa Mgombea wa 25 kujitokeza kuwania nafasi hiyo. 
Mgombea Urais wa Zanziubar wa 25 Mhe., Hasna Attai Masoud akielekea katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa Habari wa vyombombalimbali kuzungumza na kutowa Sera zake, akishindikizwa na Wapambe wake waliomshindika katika zoezi la uchukuaji wa  Fomu hiyo ya Urais wa Zanzibar. Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.