Habari za Punde

Wajasiriamali wanawake watakiwa kuitumia vyema karafuu kuzalisha bidhaa kisiwani Pemba



Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa (katika)akitazama baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasriamali kisiwani Pemba,kulia ni Asha Mussa Afisa uwezeshaji uchumi
TAMWA ofisi ya Pemba kushoto ni Sakina Bakari Ame.



Muhammed Khamis-TAMWA-Zanzibar


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA- Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amewataka wanawake wajasiriamali kisiwani Pemba kutumia vizuri neema ya zao la karafuu kisiwani humo kwa  kuzalisha bidhaa mbali mbali.

Dkt Mzuri aliyasema hayo leo wakati alipokua akitizama baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasirimaali hao kutoka Pemba huko ofisini kwake Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Alisema zao la karafuu linaweza kuzalisha bidhaa mbali mbali ambazo zinasoko kubwa ndani na je ya Nchi iwapo wajasiriamali hao wataweza kuzisanifu vyema karafuu hizo.

Akitolea mfano wa bidhaa zinazotokana na karafuu alisema ni sabuni pamoja na liwa ambalo ni maalumu na hutumika kwa ajili ya kusafishia mwili kwa wanawake na wanaume(singo)

Pia Dkt, Mzuri aliwataka wajasiriamali hao kuanza kuangaza zaidi soko la kimataifa ambapo pia kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za asili kutoka Zanzibar hususani zinazoalishwa kwa kutumia karafuu na mengineyo.

Kwa upande wake afisa uwezeshaji wanawake TAMWA ofisi ya Pemba Asha Mussa alisema wanawake wengi kisiwa cha Pemba wamehamasika na kujiunga kwenye vikundi mbali mbali vya uzalishaji wa bidhaa.

Akitolea mfano alisema pia wajasiriamali hao hawakuridhika tu na uzalishaji wa bidhaa hizo pia wameanza kujiungiza katika ufuagaji ambapo  tayari baadhi ya vikundi vinamiliki mabanda ya na wanaendelea na ufugaji
kuku.

Akizungumzia kuhusu changamoto alisema bado zipo changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika kwa wajasiriamali ambapo wakati mwengine wajasirimali hao hulazimika kukaa na bidhaa zao ndani kwa muda mrefu.

Afisa huyo uwezeshaji wanawake kiunchumi aliomba Serikali na taasisi nyengine mbali ndani ya Zanzibar na nje ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo kwa kuwa kufanya hivyo
kutawawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Akizungumzia kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa mmoja miongoni mwa wajasiriamali kutoka kisiwani Pemba Sakina Ame Bakar alisema wanajitahidi katika uzalishaji wa bidhaa  bora na zenye viwango vya hali
ya juu.

Alisema licha ya jitihada hizo lakini wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko bora na lenye uhakika kwao ambalo lingewafanya kwa wajasiriamali bora na wakimataifa.

Aidha aliomba Serikali kuendelea kuwatengezea mazingira ikiwemo kuwakutanisha na makampuni makubwa pamoja na wajasiamali wengine wa kimataifa ili waweze kutengeza masoko mapya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.