Habari za Punde

Waandishi wa Habari Zanzibar Wajitokeza Kuwania Ubunge na Uwakilishi Majimboni Kupitia CCM

Waandishi wa habari wakipongezana baada ya kukutana katika Afisi ya CCM ya Wilaya Dimani wakati wa zoezi la kuchukua Fomu za kugombea Ubunge na Uwakilishi kushoto Msangu Said anagombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki na Raya Hamad anagombea Ubunge.

Mwandishi wa Habari wa ZBC Redio Bi. Suzan Kunambi akiwa na fomu yake ya kugombea Ubunge Jimbo la Jangombe.
Mtangazaji wa ZBC TV Bi. Msangu Said mmoja wa waandishi wa habari Zanzibar waliojitokeza kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar.
Mgombea Ubunge nafasi ya Wanawake UWT Pemba mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Bi. Kauthar Is-haka akiwa na fomu yake baada ya kuchuka kwa hatua za ujazaji wa fomu hiyo.
Bi.Raya Hamad ni mmoja wa waandishi wa habari Zanzibar waliojitokeza kuchukua fomu kugombea Ubunge  akiwa na fomu yake 


1 comment:

  1. Ni aibu kwa wafanyakazi wa office za umma kujiingiza kwenye siasa, ni dhahiri vyombo vya habari haviko huru hasa hiki cha serikali

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.