Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Amefika Hospital ya MOI Jijini Dar es Salaam Kumjulia Hali Kijana Deogratius Mianga

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na mgonjwa Deogratias Mianga alipofika hospital Moi,  Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  MOI Dkt. Respicious Boniface, (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Ijumaa Julai 24, 2020) alimjulia hali kijana Deogratias Mianga mkazi wa Singida ambaye amelazwa katika Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya matibabu.

Waziri Mkuu alimuona Deogratias kupitia vyombo vya habari akiomba msaada wa matibabu kutokana na matatizo ya mgongo.  Waziri Mkuu aliguswa na hali ya Deogratius na tarehe 02/07/2020 alimuwezesha kufika MOI na kufanyiwa upasuaji tarehe 06/07/2020. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.