Habari za Punde

Sherehe za Uzinduzi wa Tamasha la Timu ya Wananchi Yanga Wazuru Kaburi la Marehemu Abeid Amani Karume Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui na Kumuombea Dua.


Mwenyekiti wa Timu ya Yanga Afrika Dr. Msindo Msolla akiwa na Wanachama wa Yanga wa Matawi ya Zanzibar wakizuru kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na kumuombea dua ikiwa na Uzinduzi wa Tamasha la Yanga Day, lililoaza leo katika Visiwa vya Unguja kwa kuomba Dua na kufungua Tawi jipya la Yanga katika Mtaa wa Kwahani na kujumuika na Wazee wa Nyumba ya Wazee Sebleni kwa chakula cha mchana na kufanya usafi katika maeneo ya Wazee.

Mwenyekiti wa Timu ya Yanga Afrika Dr. Mshindo Msolla akiongoza Ujumbe wa Wanachama wa Yanga katika hafla ya kumuombea Dua Mzee Abeid Amani Karume, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Tamasha la Yanga Day, kwa Wanachama wa Yanga Zanzibar kutoka Matawi mbalimbali yalioko Visiwani Unguja hafla hiyo imefanytika leo asubuhi katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.Wakiitikia dua ikisoma na Shekh Sharif.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.