Habari za Punde

Wadau Wa Uchaguzi Pamoja Na Wananchi Wengine Wa Kisiwani Pemba Watakiwa Kudumisha Amani Iliyopo Kisiwani Humo

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (wa pili kutoka kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman kabla ya kuanza kwa kikao kazi na wadau wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa uchaguzi kisiwani Pemba. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wadau wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa uchaguzi (hawapo pichani) leo kisiwani Pemba wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ambapo aliwataka wadau wote wa uchaguzi pamoja na wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu kwenye kisiwa hicho. Picha na Jeshi la Polisi.


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mohamed Hassan wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini baada ya kumaliza kikao kazi pamoja na wadau wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa uchaguzi leo kisiwani Pemba wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ambapo aliwataka wadau wote wa uchaguzi pamoja na wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu kwenye kisiwa hicho. Picha na Jeshi la Polisi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.