Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe,.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia Wananchi na WanaCCM alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika leo Zanzibar 3/10/2020, na kuhudhuriwa na Umati wa Wanachama wa CCM Zanzibar.
Mgombea Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Mzani Mmoja Jijini Zanzibar kuhudhuria Mkutano wa Kampeni wa CCM uliofanyika leo 3/10/2020, akiwapungia mkono Wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia wakati wa kuingia Wagombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi na Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuhudhuria mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania Mhe. Magufuli uliofanyika kayika uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo.
Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Dk. John Pombe Magufuli alipowasili katika jukwaa kuu la viongozi katika uwanja wa Mnazi Mmoja kuhudhuria mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe Dkt.Magufuli leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Mhe Dk. John Magufuli na Viongozi wengine wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Mnazi Mmoja leo 2/10/2020.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo. kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kuwahutubia Wananchi wa Zanzibar. na kuwaomba kura.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo 3/10/2020, na kuwaomba Kura na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani wote wa CCM Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar, akitangaza Sera za Chama Chake katika mkutano huo uliofanyika leo 3/10/2020.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi.(hayupo pichani) uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo 3/10/2020.
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakipiga makofi wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wananchi katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment