Habari za Punde

FURSA NYINGI ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUPATIKANA MADABA

 

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Madaba Bw. Mikael Hadu, na wataalam kutoka katika Halmashauri hiyo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao Mapema leo Wilayani Madaba.
Mchumi kutoka Halmashauri ya Madaba Bw. Bosco Mwingira akiwasilisha jambo wakati wa kikao hicho na Kulia ni Bw. Yassin Kazoba  mchumi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Picha ikionesha baadhi ya  wakulima wanawake wa Skimu ya Kilimo cha umwagiliaji cha HangaNyadinda katika kikao na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
Mwenyekiti wa Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji ya HangaNyadinda Bw.John Joakim Komba akifafanua jambo kwa wakulima wakati wa kikao na wataalam kijijini hapo.

Na Mwandishiwetu– MADABA

IMEELEZWA kuwepo kwa fursa nyingi za kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, kutokana na kuwepo kwa eneo kubwa lenye mabonde yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji licha ya maeneo hayo kutoendelezwa.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Bw.Mikaeli Hadu, alipokuwa akizungumza na wataalam kutoka Tumeya Taifa ya Umwagiliaji waliyopo katika ziara ya kikazi ya kutoa elimu na mafunzo katika baadhi ya skimu za wilaya hiyo  wakianzia na skimu ya Hanga  Nyadinda.

“Kuna fursa nyingi sana za kilimo hiki cha Umwagiliaji katika mkoa huu hasa kwa upande huu wa kuelekea Njombe, kwani mapori yanayofaa kwa kilimo ni mengi na wananchi wa maeneo haya ni wakulima wachapa kazi hivyo, Idara ya Umwagiliaji itakapokuwa katika zoezi la kuongeza eneo la Umwagiliaji ni vizuri ikaangalia maeneo haya katika jicho la kipekee na kuyaboresha, kwani wananchi wengi wamekuwa wakilima kienyeji, yaani kilimo cha vinyungu katika mabonde mengi hivyo eneo likiongezwa litahamasisha zaidi kilimo cha umwagiliaji.” Alisema.

Bw. Hadu aliendelea  kusema kuwa zipo skimu ambazo serikali imewekeza kwa ajili ya   umwagiliaji lakin iwananchi hawa zitumii vizuri kitolea mfano wa skimu ya mbanga mawe, “Serikalii na  tililia mkazo kilimo cha umwagiliaji ihivyo kuna kila sababu ya skimu hizi kufanya vizuri, wakulima wahamasishwe vya kutosha nakupewa elimuili uwekezaji huua mbao serikali imewekeza pesa nyingi ufanye kazi kwani utaboresha maisha ya wananchi.” Alisisitiza.

Akiongelea swala la migogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Madaba, Bw. Hadu alisema mkoawa Ruvuma umekuwa na uingiaji mkubwa sana wa mifugo kutoka mkoa wa Mwanza, Simiyu na Rukwa na Halmashauri hii ndiyo lango kubwa sana la kupitisha Mifugo.

 “Tumekuwa wakali sana kuhakikisha kuwa mifugo inayoingia ni yakuchinjwa na siyo ya kufuga lakini wafugaji ni wajanja wanachukua vibali kwa ajili ya kuleta ng’ombe wa kuchinja lakini wao wakiingia wanafuga, kwa hiyo tunaendelea saana kufuatilia jambo hili kwakushirikiana na Idara ya Mifugo ilikuweza kutatua migogoro inayojitokeza baina ya  wakulimana wafugaji iliwote,wasipate madhara.” Alibainisha.

Halmashauri ya wilaya ya Madaba ina skimu nne za kilimo cha umwagiliaji ambazo ni Luhimba, Ngadinda, Mbangamawe na Gumbiro zinazotajwa kuhitaji zaidi elimu kwa wakulima ambapo wataalam wakilimo cha umwagiliji walipata fursa ya kutoa elimu kuhusu Sheria ya Taifa ya Kilimo cha umwagiliaji na Mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Hanga Nyadinda..


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.