Habari za Punde

Makabidhiano ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango

Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar akitoa hotuba ya makaribisho katika Mkutano maalum wa Makabidhiano ya Ofisi na Kumuaga Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kulia) akitiliana saini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali katika Mkutano maalum wa Makabidhiano ya Ofisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kulia)akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali Nyaraka mbalimbali katika Mkutano maalum wa Makabidhiano ya Ofisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa hotuba baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali Nyaraka mbalimbali  katika hafla  maalum wa Makabidhiano ya ifisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.


NA TAKDRI ALI            MAELEZO                                                                                       

Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Mh. Jamal Kassim Ali amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo kutumia elimu walizonazo kwa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Ofisi hiyo na Taifa kwa Ujumla.

Amesema Wizara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya Wananchi hivyo ni vyema Wataalamu wa fani mbalimbali waliomo kuwa Wazalendo na kuhakikisha wanafikia malengo ya Serikali ya awamu ya nane ya kufikia uchumi wa Bluu.

Waziri Jamal ameyasema hayo huko Ofisini kwake Vuga wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa aliemaliza muda wake.

Amesema Timu ya Uongozi aliokabidhiwa ni nzuri kwani inawataalamu wengi na wa fani mbalimbali na kuahidi kuendeleza mwendo wa kasi katika kuleta maendeleo.

Aidha amepongeza Waziri huyo mstaafu kutokana na kazi na jitihada kubwa alizozichukuwa katika Uongozi wake na kuacha msingi mkubwa kwa faida ya Wizara na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri Mstaafu wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia amesema maendeleo yaliyopatikana yametokana na Ushirikiano wa Wafanyakazi wa Wizara hiyo hivyo ni muhimu kutoa ushirikiano na Waziri mpya ili kuweza kuyaendeleza na kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha amewakumbusha Wafanyakazi hao kufanya kazi kwa Uzalendo na kutosahau kuwa wanatakiwa kuwa Waaminifu na kukinai katika uwajibikaji wa kazi zao.

Nao Wafanyakazi wa Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wamemshukuru Waziri aliemaliza muda wake kwa ushirikiano aliowapa na kuahidi kushirikiana na Waziri mpya kwa maslahi mapana ya Wananchi wa Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.