Na. Beatrice Saanga-MAELEZO
Nishati
ni sekta muhimu sana kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla hususani
kuelekea katika uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika
unazalishwa na na kuwafikia wananchi
walio wengi ili waweze kufikia ndoto zao za kuanzisha na kumiliki viwanda na
kuweza kuinuka kuinua kipato cha familia zao na kuleta maendeleo ya nchi.
Aidha,
nishati ya umeme inasalia kuwa muhimu sana katika maendeleo na ukuaji
wa uchumi duniani kote hasa kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati katika matumizi ya kila siku na uzalishaji viwandani ambapo inahitajika
katika kuendesha mitambo na mikubwa na katika viwanda vidogo vinavyomilikiwa na
wajasiriamali wadogo.
Katika
kipindi cha 2019/19, Wizara ya Nishati kwa imekuwa na vipaumbele vingi hasa
katika kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unapatikana ili kuwezesha ukuaji wa
uchumi wa nchi ambapo Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imejitahidi kuongeza
uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo mradi wa kuzalisha
umeme katika Mto Rufiji ambao ukikamilika utakuwa na MW 2,100 uliopo wilayani Rufiji na miradi ya
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I - Extension MW 185,
Kinyerezi II MW 240, Somanga Fungu MW 330 ulioko mkoani Lindi pamoja na MW 300 ulioko katika mkoa wa Mtwara.
Aidha,
Serikali imeimarisha mifumo ya
usafirishaji wa umeme mkubwa nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa mradi wa
kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA),
mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi
Tanga (Tanzania) na kuendeleza miradi ya
nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na umeme-jua).
Jitihada
za Serikali katika kuimarisha nishati zimeiwezesha kutekeleza miradi mingi ya
kusafirisha umeme ambapo imepelekea kupunguza matumizi ya umeme wa mafuta na
kuwezesha kuokoa kiasi cha shilingi bilioni, 719 kwa mwaka. Mafanikio hayo
yamewezekana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia 2019/20.
Wakati
Tanzania inaelekea kutimiza azma ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kufikia
malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa katika ya Mwaka 2025 Serikali kupitia,
Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme wa MW 5,000, mwaka 2020 na kuongezeka
hadi kufikia kufikisha MW 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Mahitaji
ya umeme nchini yameendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za
kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha, wa uhakika na wenye gharama
nafuu pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme
ili kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo
mbalimbali ya nchi.
Utekelezaji
wa mradi wa kuzalisha umeme wa jumla ya MW 2,100 kwa kutumia maji (Hydro Power
Plant) katika Bonde la Mto Rufiji ni kichocheo muhimu katika kuwezesha Tanzania
kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ampapo
utekelezwaji wa mradi huu unategemewa kupunguza kama si kuondoa kabisa tatizo
la umeme nchini
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli itahakikisha inasimamia
ipasavyo na kuimarisha miundombinu ya nishati kwa kuhakikisha upatikanaji wa
huduma za umeme unaboreshwa ili kukabiliana na changomoto mbalimbali za
uimarishaji wa Mikakati ya utoaji wa huduma ya nishati ya Umeme.
Katika
hotuba yake wakati wa akizindua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma,
tarehe, 13, Novemba 2020 Rais John Pombe Magufuli alisema Serikali yake inaenda
kuwezesha upatikanaji wa umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na
umeme na kuondoa kabisa tatizo la umeme vijijini.
“Kuhusu
umeme pia, kwenye miaka mitano ijayo, tumepanga kufikisha umeme kwenye vijiji
vyote ambavyo bado havijafikishiwa umeme, ambapo idadi yake haizidi 2,384.
Kwenye miaka mitano iliyopita, kwa takwimu za hadi jana tumefikisha umeme
kwenye vijiji 9,884 kutoka vijiji 12,018 mwaka 2016. Nchi yetu ina vijiji
12,280”alisema Rais Magufuli.
Alibainisha
kuwa kwenye miaka mitano ijayo Serikali yake imejipanga kukamilisha mradi wa
ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere ambalo linategemewa kuzalisha megawati 2,115 ambapo Tanzania inakusudia
kupata umeme wa kutosha kupitia mradi huo ambao unatarajiwa kupunguza bei ya
umeme kwa wananchi.
Aliitaja
miradi mingine ambayo Serikali inakusudia kuanza ujenzi wake katika kipindi cha
miaka mitano ijayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi mingine ya umeme wa maji
Ruhudji utakaokuwa na MW 358, Rumakali MW 222, Kikonge MW 300, umeme wa gesi Mtwara
MW 300, Somanga Fungu MW 330,Kinyerezi III MW 600 na Kinyerezi IV MW 300.
Aliongeza kuwa Serikali pia inakusudia kutekeleza miradi mingine midogo midogo
ambayo kwa pamoja inakusudiwa kuzalisha umeme MW 1,100 kwa kutumia Nishati
jadidifu (jua, upepo,jotoardhi)
No comments:
Post a Comment