Habari za Punde

Umoja wa Vyama Vya Siasa visivyo rasmin vya mpongeza Rais wa Zanzibar kwa Uteuzi wa Makamo wa kwanza wa Rais

Katibu wa Umoja wa Vyama vya Siasa visivyo rasmi Ameir Hassan Ameir ampongeza Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa Uteuzi wa Makamo wa kwanza wa Rais katika mkutano na Waandishi wa Habari ulifanyika Ukumbi wa Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA / MAELEZO ZANZIBAR .

Na Maryam Kidiko  /   Maelezo Zanzibar.               10/12/2020. 

Umoja wa Vyama Vya Siasa visivyo rasmin vimempongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kumteuwa Maalim Seif Sharif Hamad  kuwa Makamo wa  Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa habari huko katika  Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar Katibu wa Umoja wa vyama vya siasa visivyo rasmin Ameir Hassan Ameir amesema hatua aloichukua Rais ni yakupongezwa na ni yakisheria.

 Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa kutimiza kauli zake za kuunda Serikali ya Kitaifa wakati wa kampeni zake .

Nae Makamo Mwenyekiti Peter Aghaton Magwira ameeleza kuwa watatekeleza kwa vitendo katika kumsaidia Rais wa Zanzibar  yale yote yanayofaa ili kuleta maendeleo katika Nchi.

 Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kufata sheria na  watamuunga mkono ili kuendeleza kuilinda amani iliyopo katika Nchi hiyo.

“Tutaendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ili kuleta maendeleo na kulinda amani ya Nchi”alisema katibu wa Umoja huo.

Vile vile waliwaomba Viongozi wote na Wananchi kwa Ujumla kushirikiana kwa pamoja ili kuzidi kuleta maendeleo ya Zanzibar . 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.