Habari za Punde

Vijana 14 Wakabidhiwa Vifaa Vya Utendaji Kazi.

Mkurugenzi Uratibu wa Shughuli za Serikali Ndg. Khalid Bakar Amran akizungumza machache wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Vijana 14 kukabidhiwa Vifaa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Jijini Zanzibar 
VijaIJANA WANUFAIKA WA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA WAKIFATILIA HUTUBA YA KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS,SERA, URATIBU NA BARAZA LA WAWAKILISHI.
WASIMAMIZI WA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA ,AKIMSIKILIZA KWA MAKINI KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ,SERA,URATIBU NA BARAZA LA WAWAKILKISHI

WANUFAIKA WA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA WAKISHUHUDIA UTOAJI WA VIFAA HUVYO.


Picha na – OMPR – ZNZ.

 



Vijana nchini wametakiwa kutokubali kukaa mitaani, badala yake wajishughulishe na shughuli za ujasiriamili , ili kujikimu kimaendeleo na kuendelea kuilinda amani ilokuwepo nchini.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,  sera, uratibu na baraza la wawakilishi Shaaban Seif Mohamed ametoa Kauli hiyo katika hafla maalum ya kuwakabidhi vifaa vya kutendea kazi kwa vijana 14 miongoni mwa walionufaika na mradi wa kuwasaidia vijana, hafla iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Dr Hussein Ali Mwinyi, imepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha vijana wanaondokana na tabia ya kukaa mitaani bila ya kujishuhghulisha na shughuli zozote za kujikimu kimaisha, kama ilivyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, badala yake  wajishughulishe  na kuondokana na fikra ya  kusubiri ajira serikalini.

Aidha katibu shaaban alisema , ni wajibu wa vijana hao kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa kwa kuthamini nguvu za serikali na      UNDP, pamoja na mashirika mbali mbali ya kimaifa yenye kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha vijana wanajikwamua na janga la ajira nchi.

Akizungungumzia suala la Elimu, Katibu Shaaban aliwataka vijana hao waliopata fursa hiyo, kuwa ni mfano kwa vijana wengine, na aliwasihi wawe mabalozi kwa wenzao katika kueleza azma njema ya serikali ya awamu ya nane katika kutatua changamoto ya ajira hasa kwa vijana, kama ilivyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ndugu khalid Bakari Amran alisema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuwa ndio wasimamizi wakuu wa watekelezaji wa ilani , hivyo ni jukumu la Wizara kusimamia suala la kuwawezesha vijana kuweza kupata fursa mbali mbali ili kuwasaidia kuweza kujikimu kimaisha.

Aidha alilishukuru Shirikila la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, kwa kulifikiria rika la vijana kwa kuwaletea mradi huu, ili kuweza kuwasaidia katika kupambana na suala la ukosefu wa ajira nchini.

Kwa upande wake mratibu kutoka UNDP, Ndugu Ali Shaibu alisema UNDP imeonelea kuwasaidia vijana katika suala la ajira, kwa kuwa tatizo hilo  huwapelekea vijana kujihusisha na matendo maovu na hatarishi amabyo kupelekea kuharibika kwa jamii.

Aidha amesema mradi huu umewasaidia vijana saba hadi sasa wanaendelea na mradi wa ufigaji kuku.

Jumla ya vijana 14 wamepatiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 15, na kupatiwa vyeti vya kumaliza masomo ya Ujasiri Amali. Katika mradi unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , chini ya usimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.