Habari za Punde

Wanaochanganya maji na mafuta vituo vya mafuta hawatovumiliwa - Waziri

 Mwashungi Tahir    Maelezo Zanzibar.   09-12-2020.

 

Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitowavumilia wamiliki wa vituo vya mafuta watakaobainika kufanya uchakachuaji kwa kunusu athari zinazoweza kujitokeza na upotevu wa Fedha za Serikali.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar  Suleiman Masoud Makame wakati alipokuwa akizungumza na Mameneja na Wamiliki wa vituo vya mafuta,huko katika ukumbi wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) uliopo Maisara Wilaya ya Mjini.

 

Amesema kuna baadhi ya Wafanyabiashara  wana tabia ya kuchanganya mafuta  jambo ambalo ni kosa kisheria na kuleta ubadhirifu .

 

Amesema Serikali ya Awamu ya nane imeahidi kusimamia tatizo la upungufu wa mafuta na kuangalia maslahi bora ya Wananchi  wake.

 

Aidha amewaasa kuacha kuuza mafuta ya magendo katika mageleni na watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria na kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kuondosha tatizo hilo.

 

Hata hivyo amewataka wadau wa mafuta kubadilika na kushirikiana katika utendaji wao wa kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

 

Kwa upande wa wadau hao wamemuomba Seikali kuwapunguzia ushuru pamoja na kuharakisha  kujengwa bohari za mafuta mpya mangapwani ili waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi.

 

Hata hivyo wamesema wanafanyakazi katika mazingira hatarishi hivyo wameomba kuwekwa utaratibu wa kupatiwa Bima ya Afya,ulinzi hasa kwa vituo vya shamba pamoja na kuangaliwa maslahi yao.

 

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.