Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said Akizungumza na Viongozi wa Skauti Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Viongozi wa Chama cha Skauti Zanzibar wakati walipofika ofisini kwake Mazizini mjini Unguja, akiwaonesha kitabu cha kusaini wageni alichokichukua katika Skuli ya Sekondari Fiedel Castro Chake chake Pemba, ambacho kilianza mwaka 1963 kikiwa na saini za Marais wote waliopita akiwemo Hayati Abeid Amani Karume.

Na Maulid Yussuf WEMA.Zanzibar

Makamo wa Rais wa Chama cha Skauti Tanzanzia Mhe Simai Mohammed Said amesema kuwepo kwa Chama  Skauti Zanzibar kutalisaidia taifa kuwa na  vijana wakakamavu pamoja na kuwa wazalendo wa nchi yao kutokana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa ndani ya Chama hicho.

Akizungumza na viongozi wa chama cha Skauti Zanzibar, ofisini kwake  Mazizini Mjini Unguja, mhe Simai amesema  upo umuhimu wa   kuboreshwa Chama hicho hapa Zanzibar ili kiweze kusikika na kutambulikana kwa lengo la kukuza vipaji vya watoto nchini.

Amesema kua suala upatikanaji wa eneo lao lina umuhimu kwani litasaidia kuwa kivutio kwa wageni na wenyeji pamoja na kuwashajiisha vijana kuweza kujiunga kwa kuweza kutanua wigo wa kuweza kujifunza masuala mbalimbali ya kikakamavu na kijamii.

Mhe Simai amesema atashirikiana na Taasisi husika katika kuona wanapata eneo lao la kudumu ili waweze kuedelea kuwaelimisha vijana kuwa wajasiri na wazalendo wa nchi yao.

Mhe Simai ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, amekitaka Chama cha Skauti Zanzibar kuwa masuala yote wanayoyafanya Skauti Zanzibar kuishirikisha Wizara ya Elimu ili kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika mambo mbalimbali kwa lengo la kuleta  maendeleo katika nchi.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar Dkt Idrissa Muslim Hija amewataka Chama cha Skauti Zanzibar kuhakikisha wanapopanga mipango yao kuiwasilisha Wizarani mapema ili kuepusha tatizo la upatikanaji wa fedha katika kutekeleza kazi zao.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu Msaidizi Skauti  TSA  Zanzibar, mwalimu Suleiman Ali Takdiir amesema wana tatizo la ukosefu wa ofisi ambapo awali walikuwepo katika Jengo la American Corner, lakini kwa sasa wamekuwa wakiazima ofisi tu kwa ajili ya kufanya shughuli zao.

Pia amesema wana tatizo la kifedha  kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa mwaka ili kupata uwakilishi wa vijana Kwa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Dodoma, hivyo amemuomba Mhe Waziri kuliangalia suala hilo. 

Katika hatua nyingine Chama cha Skauti Zanzibar katika kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi la kudumisha usafi wa mazingira nchini, kimemuhakiishia Mhe Waziri kuwa kipo tayari kujitolea kufuata agizo hilo katika maeneo mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Serikali ili kuleta haiba nzuri katika nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.