Habari za Punde

Magufuli awahakikishia wazanzibari ataendelea kuiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewainua mikono (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiri wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk, Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwake) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari Chato Mkoani Geita. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli amewahakikishia wananchi wa Zanzibar pamoja na viongozi wake kwamba ataendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha umoja na maelewano yaliopo yanaendelezwa sambamba na kuiimarisha Serikali ya Umoja wa Kaitaifa ili Zanzibar izidi kupata maendeleo.

Rais Magufuli aliyasema hayo leo katika hotuba yake fupi mara bmaana ya kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwiyi pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko Chato.

Rais Magufuli aliwapongeza viongozi hao pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kwa kuanza kuona mwanga wa maendeleo na kusema kuwa amekutana nao kutokana na viongozi hao kuwa pamoja kwani hakuna Zanzibar bila ya Tanzania.

Katika hotuba yake hiyo aliwataka Wazanzibari kuendelea kuchapa kazi na kuwahakikishia kwamba ataendelea kuwaunga mkono katika maendeleo ya Zanzibar na kamwe hatowaacha kwani ameziona jitihada zao za kuhubiri amani.

Rais Magufuli alisema kuwa hivi sasa Wazanzibari wote wanahubiri amani kutokana na kurejesha umoja wao ambapo hapo siku za nyuma hata ndoa zipo zilizovunjika kutokana na itikadi za kisiasa.

“Mambo ya vyama yasitusumbue sana kwani Maalim Seif hata  ukitaka kuja kuoa Chato, ruhusa njoo tu” alisema Rais Magufuli huku akionesha furaha aliyonayo kwa kukutana na viongozi hao.

Aidha, Rais Magufuli alieleza kuwa mara nyingi maadui wasingependa kuona Zanzibar inakuwa moja na badala yake waangependa kuweko kwa machafuko lakini viongozi wa Zanzibar wamechukua juhudi za makusudi kurejesha umoja  hasa kwa vile viomgozi wote wa Zanzibar hawana nia ya kuvunja Umoja wa Kitaifa walionao.

Alifahamisha kuwa Maalim Seif na Dk. Mwinyi wamewafanyia mema Wazanzibari na kusisitiza kwamba hivi sasa Upemba na Uunguja utaondoka  huku akiwataka viongozi hao kuendelea kuhubiri umoja.

Rais Maufuli alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kupenda umoja hasa ikifahamika kwamba yeye anatoka Unguja lakini Makamo wake wa Kwanza na Makamo wake wa Pili wote wanatoka Pemba hali ambay  inamaana kubwa katika uongozi na kumpongeza kwa kujenga upendo mkubwa.

Aliwashukuru na kuwapongeza  viongozi hao sambamba na kujadili mambo mengi zikiwemo changamoto zinazohusu maendeleo yakiwemo masuala ya ujumla ya kujenga Taifa, uimarishaji wa miradi mbali mbali ukiwemo ule wa Kigongo Musisi, ambao mapema Maalim Seif hivi leo aliutembelea.

Katika hotua yake hiyo, Rais Magufuli alitoa shukurani kwa maadhimisho mazuri ya sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yalisherehekewa kwa aina ya pekee na kupongeza viongozi hao kwa hatua hizo walizozichukua kwa kuhakikisha fedha zinatumika vizuri zaidi.

Alimpongeza Maalim Seif Sharif Hamad kwa kukubali kuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Mwinyi.

Ris Magufuli alisema kuwa uzoefu wa Maalim Seif Sharif Hamad ni mkubwa  na umajitajika katika uongozi uliopo hivi sasa Zanzibar huku akimpongeza kwa maamuzi yake ambayo ni ya kishujaa ambayo yanamaelewano ambayoni maamuzi ya Mwenyezi Mungu.

Alisema kuwa nchi nyingi duniani zinashindwa kuendelea kutokana na kutoelewana hivyo wananchi wa Tanzania na Zanzibar kwa jumla wanahitaja maendeleo na maelewano makubwa.

Rais Magufuli alimpongeza Maalim Seif kwa kuacha matakwa yake ya kisiasa na kufuata matakwa ya Zanzibar.

Alieleza jinsi anavyomfahamu Rais Dk. Mwinyi kutokana na uchapa kazi wake mkubwa na kusema kuwa anaimani kubwa kwamba Zanzibar chini ya uogozi wa Dk. Mwinyi itakuwa ya tofauti.

Aliongeza kuwa Rais Dk. Mwinyi ni jasiri, mchapa kazi na kusema kwa hatua yake ya mwanzo alioionesha katika kuiongoza Zanzibar ikiwa ni paoja na kushughulikia ufisadi  kwa kuhakikisha kila senti ya Zanzibar inatumika kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar.

Rais Magufuli alimuhakikishia Maalim Seif kwamba yuko katika Serikali salama na kwamba yuko tayari hata  kumualika akafungue mradi wowote huku akipongeza kura nyingi alizozipata Pemba na Unguja na kusema kuwa ataandaa ziara ya kutoa shukurani zake kwa usndi waliompa.

Alisema kuwa yuko pamoja na wananchi wa Zanzibar na viongozi wake na kumpongeza Rais Mwinyi kwa kuanza vizuri uonozi wake na kumtaka asiogope kutumbua majipu kwa wale wanaokwamisha miradi ya serikali na kumsisitiza aendelee.

Sambamba na hayo, Rais Magufuli alimtataka Maalim Seif kumsaidia Rais Dk Mwinyi katika kuhakikisha mali za wanyonge na Watanzania zinasimamiwa vizuri huku akieleza matumaini yake mwakubwa kwa Zazibar katika suala zima la uwekezaji.

Raais Magufuli alilipokea ombi la Dk. Miwnyi la kuweka wanyama mbali mbali katika sehemu maalum kwa vile sheria zinaruhusu ili kusudi iwe kivutio cha watalii kwa upande wa Zanzibar.  

Nae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  kwa upande wake alitoa shukurani kwa Rais Magufuli kwa kufanyika kikao hicho kilichomshirikisha yeye pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Alisema kuwa kikao hicho kilikuwa kizuri ambacho kilikuwa na madhumuni ya kuijenga Tanzania na kumshukuru Rais Mafuguli kwa utayari wake wa kufanya kazi na viongozi wa Zanzibar ambapo yeye na Maalim Seif wako pamoja katika kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Alimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa mstari wa mbele kwa kutaka Zanzibar iwe pamoja na akiwa Mwenyekiti wa CCM amekuwa akimuunga mkono katika suala zima la kuleta umoja.

Alisema kuwa Wazanzibari wote wana muelekeo wa kuwa wamoja na tofauti zao za kisiasa wamezeweka pembeneni na hivi sasa wanaijenga nchi yao.

Alitoa shukurani kwa kukutana na Rais Magufuli na kupongeza na kumshukuru kwa maelezo yake ya kwamba yuko tayari kuijenga Zanzibar ambapo hivi karibuni alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China Wang Yi ambapo aalimpa ombi la ujenzi wa barabara za kilomita 148 wenye kutumia Dola milioni 73 za Marekani ambapo kwa fedha hizo barabara nyingi za Unguja na Pemba zitajengwa na kuzisifu juhudi zake hizo.

Rais Dk.Mwinyi alimuhakikishia Rais Magufuli kwamba yeye na Maalim Seif wanafanya kila linalowezekana kuwa pamoja kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na kusema iwao wataendeda na hatua  hiyo ndani ya miaka mitano watapata maendeleo makubwa.

Alimshukuru Rais Magufuli kwa kutoa fursa hiyo ili kupanga mambo ya kusaidia kujijenga nchi na kumuahidi kwamba yeye na Maalim seif wataendelea kuleta na kuudumisha Umoja wa Kitaifa na kuijenga Zanzibar kwa mustakabali wa wananchi wote.

Aliwaeleza wananchi kwamba mazungumzo yao yametoa nguvu mpya na ari ya kuleta maendeleo makubwa na kumuomba Mwenyezi Mungu kuleta baraka zaidi katika mazungumzo hayo.

Mapema Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alitoa shukurani kwa kufika Chato na kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumshukuru kwa kuwakaribisha Chato ili  kuiona sambamba na  kupata fursa wa kutembelea mradi mkubwa wa mkakati wa Daraja la Magufuli walimtembeza na kumueleza na kueleza kuvutiwa kwake na mradi huo.

Alisema kuwa mradi huo sio tu utaunganisha mikoa mbali mbali ya Tanzania pia, utaunganisha nchi za Afrika Mashariki na kati, hivyo alimpongeza kwa muono wake kwamba mradi huo ukimalizika utakuwa muhimu sana kwa Tanzania.

Maalim Seif alimshukuru Rais Magufuli kwa kukaa pamoja na kubadilishana mawazo juu ya Tanzania na juu ya mambo ambayo yanawaunganisha Watanzania na kushauriana namna bora zaidi ya kuweza kuwatumikia Watanzania.

Alisema kuwa mazungumzo hayo yalikuwa mazuri ya kidugu ambayo yamempa matumiini kwamba Rais Magulfuli yuko pamoja na viongozi wenziwe wa Zanzibar hasa kwa kuimarisha upendo na maelewano na amefarajika kwa Rais Magufuli kusema kuwa yuko pamoja na kueleza kuwa atawaunga mkono.

Aidha, alimpongeza Rais Dk. Mwinyi na kumsifu Rais Magufuli kwa kuwapa matumaini makubwa zaidi ya kuwafanya Wazanzibari kuwa wamoja zaidi.

Mapema asubuhi Rais Dk. Mwinyi alitua uwanja wa ndege wa Chato na kupokewa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali ambapo pia alipata fursa ya kuangalia ngoma za utamaduni.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.