Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amemuapisha Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Jijini Zanzibar leo.

MTEULE Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar akisubiri kuapishwa kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo 2/1/2021 Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar,

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaaf Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwake) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Askofu wa Jimbo la Zanzibar Kanisa la TAG. Rev.Dikson Kaganga na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini Hati ya Kiapo ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, baada ya kumuapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hati ya Kiapo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, baada ya kuisain, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar baada ya kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) na (kulia kwake) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaaf Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati wa hafla hiyo.
WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Katibu  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 2/1/2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.