Habari za Punde

Uzinduzi wa Matembezi ya Hiyari ya Umoja wa Vijana wa CCM kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mh. Hemed Suleiman akisalimiana na Viongozi wa CCM alipofika katika Kijiji cha Pwani Mchangani kuyazindua Matembezi ya Hiyari ya Umoja wa Vijana wa CCM kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla na Viongozi wengine wakiyasubiri Matembezi ya Vijana ili kuyazindua rasmi katika Uwanja wa Michezo wa Buruda Pwani Mchangani Mkoa Kaskazini Unguja.
Mheshimiwa Hemed Suleiman akipasha mwili na Viongozi wengine wa CCM katika siku maalum ya kuyazindua Matembezi ya Hiyari ya Umoja wa Vijana wa CCM Huko Pwani Mchangani.


 Vijana wa UVCC wakihamasika kupasha mwili kwa ajili ya kuanza kwa Matembezi yao ya kuadhimisha shereha zi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 57.
Kundi la Umoja wa Vijana wa CCM wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi aliyefika Pwani Mchangani kuwazindulia Matembezi yao ya Hirari kuadhimisha Shereh za kutimia Miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kundi la Umoja wa Vijana wa CCM wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi aliyefika Pwani Mchangani kuwazindulia Matembezi yao ya Hirari kuadhimisha Shereh za kutimia Miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Nd. Mwalim Rymond Mangwala akitoa Taarifa kuhusiana na Matembezi hayo ya hiyari ya UVCCM.
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Zanzibar Mh. Tabia Maulid Mwita akitoa salamu kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa matembezi ya hiari yaliyoshirikisha Vijana 700 kutoka Wilaya zote za Zanzibar na baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara.
 Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mh. Hemed Suleiman akizungumza na Vijana wa UVCCM wakati akiyazindua rasmi Matembezi hayo ya hiyari ya Vijana.
Mheshimiwa Hemed Suleiman akikabidhi Picha ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar  Marehemu  Mzee Abeid Amani Karume Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM kwenye Matembezi ya Hiari ya Umoja huo.
Mheshimiwa Hemed Suleiman akikabidhi Bendera ya Chama cha Mapinduzi {CCM}kwa Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM kwenye Matembezi ya Hiari ya Umoja huo.

 Mheshimiwa Hemed Suleiman akiukabidhi Bendera ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM kwenye Matembezi ya Hiari ya Umoja huo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema ni wajibu wa Vijana wa Kizazi cha Sasa kutafsiri kwa vitendo maana halisi ya Uhuru wa Taifa lao  kwa kuleta Mapinduzi ya Kiuchumi yatayokwenda kwa kasi kubwa Zaidi ili kuleta ustawi.

Akiyazindua  Matembezi ya hiari ya Umoja wa Vijana wa CCM ya kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Uwanja wa Buruda katika Kijiji cha Pwani Mchangani yaliyoshirika Vijana kutoka Wilaya zote za Zanzibar pamoja na baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara alisema Vijana wana nafasi kubwa katika kulitumikia Taifa na kuleta Maendeleo.

Alisema Historia inaonyesha wazi kwamba nguvu na ari za Vijana ndizo zilizotumika kukamilisha Ukombozi. Hivyo Vijana wa Kizazi Kipya  ni muhimu kwao kujitambua na kujiweka imara katika kufanikisha malengo ya ukombozi wa kweli wa Jamii Nchini.

Alifahamisha kwamba endapo Vijana wataendelea kushirikiana vyema na kusaidiana katika kutafuta na kutengeneza ajira zile changamoto zilizowazunguuka ndani ya Jamii zinaweza kutatuka kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Hemed Suleiman ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka mfumo mzuri wa upatikanaji wa ajira kupitia Sekta ya Umma na zile Binafsi ambazo humuwezesha Kijana kuwepuka mambo maovu.

Aleleza kuwa Serikali Kuu imedhamiria kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwas makundi yote ya Vijana kwa lengo la kuhakikisha inawapatia fursa za ajira kwa namna iliyo bora na sahihi kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo Nchini.

Mheshimiwa Hemed amelipongeza Kundi hilo la Vijana  kwa uamuzi wao waliouchukuwa kupitia Matembezi hayo ya hiari ya Siku Nane zitakazojumuisha pia shughuli tofauti za Ujenzi wa Taifa na kujijenga katika Uzalendo na Utii wa kupigania maslahi mapana ya Taifa.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwakumbusha Vijana hao kuwa tanuri la kuwafinyanga wenzao mitaani kujiepusha na vitendo rushwa, wizi, Ubadhirifu na uzembe unaoviza Maendeleo yao.

Aliuagiza Uongoziwa Halmashauri zote lazima uhakikishe unapatikana usalama wa kutosha wa msafara Vijana hao kila watakapopita na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Akisoma Risala ya Matembezi hayo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar Nd. Mussa Haji Mussa alisema jumla ya Vijana Mia Saba wanashiriki Matembezi hayo yanayotarajiwa kuchukuwa umbali wa Kilomita 769.8.

Nd. Mussa Haji alisema Kundi kubwa la Vijana katika maeneo mbali mbali Nchini wanaunga mkono jitihada kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali Kuu zikiwa na kasi kubwa ya matumaini katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake Mijini na Vijijini.

Alimthibitishia Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauti Kuu ya Taifa ya CCM kwamba Vijana wa Zanzibar wameahidi kuunga mkono jitihada hizo za Serikali kwa kufanya kazi katika misingi ya Uzalendo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.