Habari za Punde

NAIBU WAZIRI KATAMBI AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WCF

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi, akitoa hotuba ya uzinduzi. Kulia ni MKURUGENZI Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. 

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi amezindua Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kutoa wito kwa wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii kwani ndio nguzo kuu katika mafanikio ya Mfuko.

Mhe. Katambi ameyasema hayo mjini Morogoro leo Februari 10, 2021 wakati akizindua baraza la Wafanyakazi WCF kwenye ukumbi wa Magadu.

“Lazima tujue uwajibikaji ni nguzo kuu ya mafanikio katika sehemu yoyote ya kazi, hivyo wajumbe mnaowawakilisha wafanyakazi wa Mfuko mnapaswa kuwahimiza wenzenu kuhusu  swala hilo.” Alifafanua  Mhe. Katambi.

Alisema Serikali inatambua mchango wa wafanyakazi wote nchini lakini vile vile inatambua sana  na kuheshimu mchango wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi katika kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya wafanyakazi wanaougua au kuumia kutokana na kazi haipotei kwa wakati wote kupitia huduma ya matibabu inayotolewa kwa waathirika.

“Napenda niwahakikishie kuwa Serikali ya awamu ya tano inaendelea kushirikiana na Mfuko katika kuhakikisha unanufaisha watu walio wengi na kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake.”

Naibu Waziri Katambi pia aliupongeza Mfuko huo kwakuwa na wafanyakazi wachache lakini waliouwezesha Mfuko kupiga hatua kubwa katika utekelzaji wa majukumu yake.

“Mnatupa heshima kubwa sana Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri mama Jenista Mhagama, tangu mmeanza kutekeleza majukumu haya mmeanzia ziro baada ya mwaka mmoja mkalipa shilingi bilioni 1.5 na bado mnaendelea kufanya vizuri kwakweli habari hizi zilifurahisha na hata kamati ya bunge ilishukuru na kuwapongeza hongereni sana sana.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Katambi.

Alisema hata baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge wametoa ushuhuda jinsi Mfuko huo umekuwa ukihudumia vema katika suala la fidia na HUDUMA za utengamao (rehabilitation aervices).

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba alisema katika kipindi cha miaka sita ya uhai wa Mfuko kumekuwepo na mafanikio kadhaa chini ya nguvu kazi ya wafanyakazi 129 ambao wameweza kutekelza vema majukumu yao

“Sambamba na hilo tumekuwa tukiwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledi katika utendaji wa kazi.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Bw. Mashomba pia alisema miongoni mwa maeneo ambayo Mfuko umeboresha sana HUDUMA zake  ni kuweka mfumo wa utoaji taarifa kwa njia ya mtandao.

“Huduma zetu hivi sasa zinatolewa kwa kiasi kikubwa sana kwa njia ya mtandao karibu asilimia 85 ya shughuli zetu, kujisajili, kuwasilisha michango, uchatakati wa malipo lakini pia muhimu zaidi ni kutoa taarifa pale mfanyakazi anapougua au kupata ajali ya kikazi na hata inapotokea bahati mbaya akafariki kutokana na kazi tumeweka mfumo mzuri unaowezesha taarifa hizo kutufikia kwa haraka kupitia mtandao.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Alisema Mfuko unatambua kuwa nchi ni kubwa na sio sehemu zote mtandao unapatikana kwa urahisi hivyo Mfuko umefungua ofisi za kikanda, kuna ofisi Makao makuu ya Serikali Dodoma, Mbeya, Arusha, Morogoro, Mtwara na mwisho wa mwaka huu wa fedha Mfuko utafungua ofisi kwenye mikoa ya Tabora, Geita na Shinyanga hususan maeneo ya migodi kama Kahama.

“Ukiacha hayo Mfuko wetu kifedha tumejenga uwezo wa kutosha kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa na CAG tarehe 30/06/2020 tulikuwa na ukubwa wa thamani (Assets) wa Bilioni 333, lakini pia hesabu ambazo hazijakaguliwa na CAG hadi Desemba 2020 tumefikia bilioni 389.” Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Mshomba.

Lakini pia Mfuko umeboresha sana huduma za tathmini kwa kutoa mafunzo kwa madaktari wapatao 1,085 ambao ndio wanaofanya kazi ya kutathmini pale mfanyakazi anapougua au kuumia kutokana na kazi.

Naye Katibu Mkuu wa  chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Heri Mkunda alisema Mafanikio yaliyopatikana WCF ni kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma kushauri vizuri uongozi na kushirikishwa katika masuala mbalimbali yanayohusu taaisi.

“Niipongeze Menejimenti na kuwaomba waajiri wengine kujifunza kutoka WCF, hawa wafanyakazi ndio walio jikoni wanaweza kushauri vizuri kuhusu masuala mbalimbali inayohusu taasisi ili kufikia malengo.”

Awali kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, wajumbe walifanya uchaguzi wa kuchagua Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi, ambapo Bw.Mbarikiwa Masinga alichaguliwa kuwa Katibu wa Baraza na Bi.Irine Mngure alichaguliwa kama Katibu Msaidizi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akipeana mikono na MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa WAFANYAKAZI (WCF) Bw. Masha Mshomba Mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko huo mjini Morogoro Februari 10, 2021. Anayeshuhudia ni Karibu Mkuu wa TUGHE Bw. Heri Mkunda
Baadhi ya wajumbe wa baraza la Wafanyakazi WCF wakishangilia kwa kupiga makofi.
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (wapili kulia) akimkabidhi Katibu wa Baraza Hilo Bw.Mbarikiwa Masinga Mkataba Kati ya Baraza na Menejimenti huku Katibu Msaidizi Bi. Irine Mngure akishuhudia.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi, (katikati) na Karibu wa Baraza la Wafanyakazi WCF, Bw. Mbarikiwa Masinga wakimsikiliza MKURUGENZI Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba wakati akitoa hotuba take.
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Bw. Julius Lwenje akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mhe. Katambi (kulia) na Bw. Mshomba wakiimba wimba was solidarity forever
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya WCF.
Picha ya pamoja ya wajumbe na mgeni rasmi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.