Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amesaini Kitabu cha Maombolezi Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini Kitabu cha maombolezi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar leo 23/2/2021.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Tukio hilo limefanyika leo huko katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar ambapo Rais Dk. Mwinyi alisaini kitabu hicho mnamo majira ya saa tatu za asubuhi leo.

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alifariki dunia mnano Februari 17,2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar-es-Salaam na kuzikwa huko kijijini kwao Nyali Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.