Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya ZBC.

 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amemteua  Dk. Ali Ahmed Uki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Rais Dk. Mwinyi amemteua Mwenyekiti huyo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 8 (1) (a) cha Sheria ya Shirika la Utangazaji Namba 4 ya mwaka 2013.

Uteuzi huo umeanza tarehe 05 Februari, 2021.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.