Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria kukipokea rasmi kivuko kipya cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU ambacho amekipokea leo kutoka kwa makandarsi Songoro Marine Transport Boatyard katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.
Kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU kikielea majini mara baada ya kupokelewa rasmi leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katikati akipewa maelezo na nahodha wa kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU wakati akikagua kivuko hicho mara baada ya kukipokea rasmi leo hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo akisisitiza jambo wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV.
KILINDONI HAPA KAZI TU, hafla iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani.
Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria
200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na
Nyamisati.
Kivuko hicho kipya kilichogharimu shilingi Bilioni 5.3 mpaka kukamilika kwake na ambacho ujenzi wake umegharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani, kimejengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ya jijini Mwanza katika karakana yake ya kujengea na kukarabati vivuko iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 ambazo ni sawa na tani 100.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea kivuko hicho iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa kadha wa mkoa huo, mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuweza kutoa fedha zote hizo kwa ajli ya kuhudumia wananchi wake na pia aliupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kuweza kusimamia ujenzi wa Kivuko hicho hadi kukamilika kwake.
‘’Kama mlivyosikia katika hotuba
zilizotangulia Wakala umekamilisha miradi ya ujenzi wa vivuko vipya vya Kayenze
– Bezi, Bugolora - Ukara na Chato – Nkome na kufanya vivuko vipya
vilivyonunuliwa katika mwaka wa fedha 2019/20 kuwa vinne kikiwepo hiki cha
Kilindoni tunachokipokea leo kwa pamoja vikiwa vimegharimu jumla ya Shilingi bilioni 15.3. Haya yote ni
matunda ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya tano chini
ya Jemedari wetu Mheshimiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli, rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.’’
Alisema Mheshimiwa Ndikilo ambapo
aliongeza kuwa kwa kuwa Kivuko hicho ni
rasilimali muhimu ya Taifa na kinahitajiwa na wananchi wa Mafia na Nyamisati, aliuagiza
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia kwa karibu uendeshaji wake ili
wananchi wafaidi matunda mazuri ya Serikali yao kwa fursa ya maendeleo yao
binafsi na nchi nzima kwa ujumla wake na pia aliwasisitizia wananchi wa Mafia
na Nyamisati kukitunza kivuko hicho na kuwapa ushirikiano wa kutosha wahudumu
wake kiweze kuwahudumia kwa kipindi kirefu.
Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara
ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga, Mhandisi Elizabeth Manzi akizungumza katika
hafla hiyo, amesema ni dhamira ya Serikali kutaka kutoa huduma iliyo bora
yenye kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania na Katika mwaka wa fedha 2019/20, Serikali
ilitoa jumla ya Billioni 12,245,214,800.00
kwa ajili ya miradi ya vivuko na maegesho ambayo inatekelezwa na Wakala wa
Ufundi na Umeme na Fedha hizo zinatokana na Mfuko Mkuu wa Serikali na Mfuko wa
Barabara.
Awali,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle,
akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa kivuko hicho alisema, kazi ya ujenzi huo imefanywa kulingana na viwango vinavyokubalika Kimataifa (IMO Standards).
‘’Kivuko
hiki kimefanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi na Shirika la Uwakala
wa Meli Tanzania (TASAC) ambao walikuwa wakishiriki ukaguzi wakati wa
ujenzi ili kuthibitisha viwango vya usalama wa abiria, magari na mizigo.’’ Alisema
Mhandisi Maselle ambapo aliongeza kuwa baada ya ukaguzi wa mwisho TASAC wamefanya usajili
wa kivuko hiki kabla hakijaanza kazi kwa
jina la MV KILINDONI – HAPA KAZI TU.
‘’Ili kuhakikisha usalama wa kivuko hiki kinapofanya
kazi kimefungwa vifaa stahiki vya kuongozea kama vile Radar, GPS, Echo Sounder, vifaa vya mawasiliano (Communication
equipment) na vifaa vya uokoaji vya kutosha kwa watu wazima na watoto ambavyo
ni makoti ya kujiokoa (life
jackets) na maboya (life rafts na life buoys).’’ Alimaliza Mtendaji Mkuu ambapo
alishukuru Serikali
kwa kuendelea kuuamini Wakala katika kutekeleza miradi hiyo na pia kuendelea
kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za
usafirishaji katika maeneo mbalimbali nchini na kuahidi kukitunza kivuko hicho
kwa kukifanyia matengenezo kama inavyotakiwa ili kiweze kudumu na kutoa huduma
bora kwa wananchi kwa wakati wote.
Kukamilika kwa ujenzi wa kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU kunafanya idadi ya vivuko kote nchini kufikia 33 hadi hivi sasa na hivyo kuifanya serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri kwa manufaa ya wananchi wengi.
No comments:
Post a Comment