Habari za Punde

Timu ya Nyaishozi FC Yapokea Udhamini wa Jezi na Fedha, DC Mheruka Amewaomba Wananchi na Wadau Kuendelea Kuichangia Timu Yao.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea jezi kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea kiasi cha pesa kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.

Na. Eliud Rwechungura.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka amewaomba wadau na wananchi wa mkoa Kagera kuendelea kuichangia timu ya Nyaishozi FC ambao ni mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo imepagwa kundi D na itachezea mechi katika kituo cha Katavi.


Mheruka ameyasema leo, Machi 01, 2021 alipokuwa akipokea jezi za wachezaji na pesa ya kuisaidia timu kutoka kwa kambuni ya Hlucky Kombucha investment ambao ni wazalishaji wa kinywaji cha Kombucha Ginger Drink ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishizi FC.


‘‘Nitoe wito kwa Wananchi wote na wadau waendelee kuichangia timu yetu Nyaishozi, Timu hii imetutoa kimaso maso ni timu ambayo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Kagera lakini pia niwashukuru umoja wa Wanakaragwe wanaoishi Dar es salaam nao wanaendelea kufanya michango yao kupitia WhatsApp pia Jambo Bukoba ambao tumeshapokea michango yao”


Mheruka ameendelea kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambae amekuwa mstali wa mbele kwa kujitoa kuiwezesha timu hiyo pia kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya Karagwe pia  ameonekana akiandaa matamasha mbalimbali ya kutafuta na kuinua vipaji vya vijana ndani ya wilaya Karagwe.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne amesema kuwa Kampuni yake imeamua kuunga mkono timu ya Nyaishozi FC ili kuunga mkono michezo ndani ya mkoa lakini pia kuumunga mkono Rais wetu pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ndie Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwa sababu tuna timu ambayo imewakilisha wilaya Karagwe vizuri na sasa inaendelea kuuwakilisha Mkoa vizuri katika ligi ya Mikoa (RCL2021)


Aidha, Bw. Hamis Jumanne ameendelea kuihakikishia timu ya Nyaishozi FC kuwa atakuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kuunga mkoa timu hiyo ili iweze kushinda katika ligi ya mikoa ili hata wilaya ya Karagwe tupate hata timu ya Kutuwakilisha katika ligi Daraja la pili panapo majaliwa.


Naye, Kocha Msaidizi wa timu ya Nyaishozi Fc, Jonson Majara amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Karagwe na mkoa wa Kagera kuwa tayali timu ipo kambini na imeshajipanga vizuri kwa kushirikiana na benchi la ufundi na uongozi wa timu kuhakikisha inarudi na ushindi ili angalau mkoa upate timu ya pili inayocheza ligi katika daraja la juu, itapendeza sana kwasababu timu hii ni timu ya wanannchi ukizingatia namna ambavyo wanaendelea kujitoa kwa ajili ya timu hiyo.

 

Awali, Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said amewashukuru wananchi na wadau wote wanaoendelea kujitoa na kuunga mkono timu ya Nyaishozi maana timu bado ni changa kushiriki ligi hizi na amehaidi atashirikiana na timu kuhakikisha inapata ushindi katika ligi hiyo inayoanza Machi 04, 2021 huko mkoani Katavi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.