Habari za Punde

ZANTEL Yazindua Ofa ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Ndg.Mohammed Khamis Mussa (Katikati) pamoja na Mkuu wa biashara wa Zantel, Bi.Aneth Muga (Kulia) na Meneja wa Masoko Bi.Rukia Mtingwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani inayowawezesha wateja kuwasiliana zaidi na kupata maudhui ya kiislamu kama nukuu za Quran tukufu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha kufanikisha funga zao. 

Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Ndg.Mohammed Khamis Mussa akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ya Zantel inayowapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na maudhui ya Kiislam kama nukuu za Quran Tukufu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha waislamu kufanikisha funga zao.Kulia ni Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar Bi.Rukia Mtingwa.

Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Bi.Rukia Iddi Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani inayowapa wateja uhuru wa kusaliana zaidi pamoja na maudhui ya kiislamu kama nukuu za Koran takatifu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha waislamu kufanikisha funga zao. Kushoto ni Mkuuwa Zantel-Zanzibar Ndg.Mohammed Khamis Mussa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.