Habari za Punde

MAJALIWA AZINDUA KITABU CHA MKAKATI WA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA 2022

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma, Mei 22, 2021.  Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu , wa tatu kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Albina Chuwa na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mayasa Mwinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,  Hemed Suleiman Abdulla wakiwa wameshika mfano wa Kitabu katika Uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwenye viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma, Mei 22, 2022. Kulia ni Mtakwimu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Albina Chuwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi nakala ya kitabu  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA, Jacqueline Mahon katika uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya  Mwaka 2022  kwenye Viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma, Mei 22, 2021. Kushoto ni  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleima Abdulla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Kitabu cha Mkakati  wa Usimamizi  na Utekelezaji wa  Sensa ya Watu na Makazi  ya Mwaka 2022, kwenye viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma,
Baadhi ya washiriki wa Uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 wakimsikiiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika uzinduzi huo kwenye viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa Uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 wakimsikiiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika uzinduzi huo kwenye viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla  katika Uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Hemed Suleiman  Abdulla  baada ya kuzindua Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na  Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022  kwenye Viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma, Mei 22, 2021.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na wa tatu kulia ni  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.