Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mpango Atembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimpa pole na kumfariji Bibi Leah Mahibwa (50) Mkazi wa Manyoni aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei 04,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na kuwapa pole Wananchi mbalimbali waliofika  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa Matibabu wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa mambo ya Neuron Surgery Dr. Humba, kuhusu maendeleo ya Matibabu ya Bibi Zaveria Chuga Malamba (62) Mkazi wa Dodoma aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo
Picha na OMR.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.