Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Aliyowaandalia.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Salum Gharib baada ya kumalizika kwa Sala ya Magharibi iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mkokotoni, wakati wa hafla ya futari ilioandaliwa na Rais kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari Maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mkokotoni, (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud
WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika Futari Maalum iliandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni Unguja
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na kutowa salamu za Mkoa wakati wa hafla ya Futari Maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya Msahafu uliotolewa na Masheikh wa Mkoa wa Kaskazini Unguja akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa kwa Wananchi wa Mkoa huo.
KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni Unguja, akimuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na (kushoto kwake ) Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Mhe Mtumwa Peya Yussuf
WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni
WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni
MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Ali Akalipo Ali akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya fitari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa huo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya futali maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni.
BAADHI ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya futari aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa huo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni
BAADHI ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya futari aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa huo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni.
 MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliofanyika katika ukumbo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ,Sera,Uratibu wa Baraza la Wawakilishi.Dkt.Khalid Salum Mohammed

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.