Habari za Punde

Kampuni ya SD Biosensor ya Korea Yakabidhi Msaada wa Vifaa vya Uchunguzi wa Covid 19 kwa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akikabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea akikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vital Supplies Limited ya Tanzania Bw. Jimmy C Apson. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na (kushoto kwa Makamu) Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Mkurugenzi) CEO wa Vital Supplies Limited Bw.Sanjay Patadia wakipika makofi wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Bw. Jimmy C. Apson na CEO wa kampuni hiyo Bw. Sunjay.Patadia wakiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya Vipimo vya Uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolewana Kampuni ya SD.Biosensor ya Korea.

CEO wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Tanzania Bw.Sanjay Patadia akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vifaa vya Maabara vya Uchunguzi wa Covid 19 kwa Wizara ya Afya Zanzibar, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor kutoka Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

BAADHI ya Madaktari na Maofisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifutilia hafla ya kukabidhi Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid -19, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbiu wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akizungumza na kutowa maelezo ya makabidhiano ya Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolena Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar. Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea kwa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto  Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara kwa ajili ya Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, kwa ajili ya uchunguzi wa Covid 19, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

CEO wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Bw.Sanjay Patadia akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, akizungumza na kutowa shukrani kwa Kampuni ya SD.Biosensor ya Korea kwa kutowa msaada huo wa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi Covid 19,kwa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

















Na Miza Kona Maeleao Zanzibar   21/05/2021


Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman ameitaka jamii kufuata miongozo ya afya na kuongeza hamasa ya mapambano ili kujikinga ugonjwa wa Corona nchini.


Makamu wa Kwanza ameyasema huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika hafla Makabiadhiano ya Vifaa vya haraka vya kupimia Virusi vya Corona, amesema  ni jukumu la kila mtu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo .


Amesema Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua jitihada kubwa ya kupambana na ugonjwa Corona nchini, vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya kiwango cha  upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika jamii.


Amefahamisha ugonjwa wa Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa duniani hivyo ni vyema kushirikiana wafadhili na wadau mbalimbali katika kujenga miundombinu mizuri ya afya ili kuepukana na maambukizi.


Makamu wa Kwanza amewasisita wafanyakazi wa wizara ya afya kuitumia vyema msaada huo kwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Akizungumzia kuhusu hali ya maambukizi nchini Makamu wa kwanza amesema kuwa ugonjwa upo lakini hali sio mbaya hivyo amewasisitiza wananchi kuwa watulivu na kutosikiliza taarifa potofu zinazotolewa katika mitandao ya kijamii ili kuepuka taharuki.


Nae Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto mhe. NassorAhme Mazrui amesema ugonjwa Corona ni tishio duniani  ni vyema jamii kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi .


Amefahamisha kuwa vifaa hivyo vya kupimia virusi vya Corona ni vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo hutoa majibu ya papo kwa papo vitasaidia kugundua kwa haraka wale wenye kupata maambukizi ya ugonjwa huo.


 Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Supplier CEO Sunjay  C. Patadia amesema kampuni yake ina uwezo wa kutengeneza dawa na vitendakazi vyevye ubora kimataifa na vifa vipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii bila madhara.  


Vifaa hivyo vya haraka vya  kupimia Virusi vya Corona vyenye thamani ya Tsh. Milioni 250 vimetolewa na Kampuni ya SD BIOSENSOR na SUPLIER CEO kutoka Korea

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.