Habari za Punde

ZEC yazitaka Taasisi zilizoangalia uchaguzi Mkuu 2020 kuwasilisha ripoti zao

Mkurugenzi wa ZAFAYCO ABDALLA ALI ABEID akitoa maelezo mafupi juu ya ripoti ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020 Kutoka Jumuiya ya ZAFAYCO wakati wa kuwasilisha Tume ya uchaguzi ya Zanzibar leo tarehe 21 Mei, 2021

Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC Mhe. Mabruki Jabu Makame kulia akipokea ripoti ya Waangalizi wa Uchaguzi Kutoka Jumuiya ya Kupambana na changamoto za Vijana Zanzibar ZAFAYCO iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa ZAFAYCO  tarehe 21 Mei, 2021  katika ukumbi wa Mikutano wa ZEC Maisara Mjini Zanzibar ( Picha na Jaala Makame Haji - ZEC)

 

Na Jaala Makame Haji - ZEC

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imezitaka Taasisi zilizozoshiriki kuangalia Uchaguzi Mkuu kuwasilisha ripoti zao za uangalizi kwa kutoa mapendekezo yenye nia ya kujenga Amani na utulivu na kutanguliza  maslahi ya wananchi kuliko kueleza zaidi hisia za kisiasa

Ushauri huo ulitolewa na Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe. Mabruki Jabu Makame katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume hiyo Maisara Zanzibar mara baada ya kupokea ripoti ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020 kutoka Jumuiya ya kupambana na Changamoto za Vijana Zanzibar ZAFAYCO

Makamo Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa Changamoto na Mapendekezo yaliyowasilishwa katika ripoti za uangalizi zina lengo la kumarisha uendeshaji na Usimamizi wa Chaguzi zijazo

Hata hivyo, ZEC imezipongeza Taasisi za ndani ya nchi zilizoshiriki kuangalia Uchaguzi Mkuu 2020 kwa kuwa wa Mwanzo kutoa matamko juu ya mwenendo wa Uchaguzi kuliko taasisi za nje ya nchi hali ambayo ni tofauti na chaguzi zilizopita.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya ZAFAYCO Abdalla Ali Abeid alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar katika kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu 2020 kwa vile Tume hiyo iliyashirikisha kwa karibu zaidi makundi ya Vijana kushiriki katika harakati za Uchaguzi.

Ndugu Abdallah alieleza kuwa, ZAFAYCO iliridhishwa na uamuzi wa ZEC wa kuondosha ukomo wa idadi ya Waangalizi kwa taasisi za Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020 hali ambayo iliufanya Uchaguzi Mkuu 2020 kuwa huru na wazi katika hatua zote kuanzia Uandikishaji hadi upigaji kura

Taasisi ya kupambana na changamoto za Vijana Zanzibar ZAFAYCO imewasilisha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ripoti ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020 uliofanywa na Waangalizi kutoka Taasisi hiyo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.