Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP
David Misime akipokea taarifa maudhurio ya waandishi wa habari wa Polisi kutoka
kwa ASP Richard Minja yaliyofanyika
katika Shule ya Polisi Moshi yenye lengo la kuwajengea Mweledi maafisa habari
wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi
Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP
David Misime katikati kwa waliokaa na kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Polisi
Moshi SACP Ramadhan Mungi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa, wakaguzi
pamoja na askari walioshiriki mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa
Polisi nchini yaliyofanyika katika katika
Shule ya Polisi Moshi yenye lengo la
kuwajengea Mweledi maafisa habari wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi,
Mikoa na Vikosi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi
SACP David Misime mapema leo amefungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa
habari wa Polisi nchini yaliyofanyika
katika Shule ya Polisi Moshi yenye
lengo la kuwajengea weledi wakutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku ikiwa
ni pamoja na kuongeza ushirikiano na wadau wengine. Maafisa habari hao wa Jeshi
la Polisi ni kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi.
Misime amesema wandishi
hao wanafanya kazi katika ofisi za Makamanda
wa Polisi mkoa na vikosi wakiwa na majukumu ya kuwasaidia Makamanda kwenye
shughuli zote za kihabari ikiwemo kuandaa taarifa kwa vyombo vya habari (Press
Releases) ama Press Conferences lakini
kutengeneza Dokumentari mbalimbali ambazo zitatumika kutoa elimu kwa jamii.
Aidha Msemaji wa Jeshi la
Polisi David Misime aliwataka waliohudhuria mafunzo hayo kushiriki kikamilifu
kwa kusikiliza, kuuliza maswali ili kuwa na weledi zaidi katika utendaji wa
kazi za kila siku.
Misime alitaja mambo
ambayo watafundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja namna ya kuundaa na kutoa
taarifa kwa waandishi wa habari, mahusiano kati ya waandishi polisi na wadau
wengine, namna kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, namna
ya kuripoti makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto,mapambano
ya kisaikolojia na habari ambapo kwa ujumla mada zitakazo tolewa ni 14.
Msemaji wa Jeshi la
Polisi SACP David Misime alimshukuru mwakilishi wa LSF Fortunata Ntwale (Afisa
Program) kwa ushirikiano uliowezesha mafunzo hayo kufanyika.
Naye Afisa Program
kutoka LSF Fortunata Ntwale katika ufunguzi huo amesema wamefadhili mafunzo
hayo ili kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwajengea uwezo wanahabari wao wa
kutoa elimu katika kutetea haki za watoto na wanawake kwa kushirikisha wadau
wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment