Habari za Punde

Michuano ya UMISSETA Mkoani Mtwara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (aliyejishika kidevu) akiangalia mechi ya nusu fainali baina ya timu ya Mtwara na Dodoma ambapo Mtwara imeshida bao 1 na Dodoma 0. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya kuchoto ni Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo.

.Mchezo wa nusu fainali wa Michuano ya UMISSETA inayofanyika Mkoani Mtwara kati ya Dodoma na Mtwara mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mtwara.Timu ya imeshinda mchezo huo kwa bao 1-0.

Golikipa wa Timu ya Geita akijaribu kuokoa moja ya peneti ikipigwa na mchezaji wa Timu kutoka Pemba wakati wa michezo ya kuwania Kombe la UMISSETA uliofanyika katika uwanja wa mtwara timu ya Pemba imeshinda mchezo huo kwa Penenti dhidi ya Timu ya Geita kwa 4-3. 

Mwandishi Maalum, Mtwara

Michezo inayoendelea kwenye Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) yanafikia fainali Julai 1, 2021 kwenye viwanja mbalimbali vya mjini Mtwara ambapo mashindano hayo yatafungwa rasmi Julai 2,2021.

Kwa mujibu wa Msemaji wa mashindano hayo, John Mapepele fainali ya soka kwa wavulana itakuwa baina ya timu ya Pemba na Mtwara na itachezwa siku ya kufunga mashindano hayo Julai 2, 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu soka utachezwa kesho baina ya timu ya mkoa wa Dodoma na Geita.

Amesema mchezo wa Soka kwa upande wa wasichana utakuwa baina ya timu ya mkoa wa Mwanza na Tabora ambao utachezwa mchana Julai 1,2021 ambapo hadi sasa mshindi wa tatu ni mkoa wa Arusha.  

Pia fainali ya Mpira wa Pete itakuwa dhidi ya timu ya mkoa wa Mwanza na Songwe

Kwa upande wa mpira wa Wavu fainali wasichana itachezwa baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara wakati wavulana itakuwa kati ya Dar es Salaam na Arusha.

Mpira wa mikono fainali wasichana itakuwa baina ya mkoa wa Songwe na Morogoro na kwa upande wa wavulana Unguja watakipiga na Tabora.

Kwa upande wa mpira wa kikapu fainali kwa wanaume itakuwa baina ya Unguja na Dar es Salaam wakati kwa upande wa wanawake itakuwa baina ya Dar es Salaam na Mwanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.