

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametaja hatua zitakazochukulia na
Tanzania katika kuboresha haki za kiuchumi kwa wanawake.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika
Paris Ufaransa.
Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Tanzania
inachukua hatua muhimu ili kukuza na kulinda haki za kiuchumi kwa wanawake.
Mheshimiwa Makamu wa Rais
amezitaja hatua hizo ni pamoja nakuongeza vituo vya kulea watoto mchana katika
maeneo mbalimbali ya shughuli za kiuchumi kama vile sokoni na maeneo mengine ya
kazi .
Makamu wa Rais amesema
serikali inachukua hatua za kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii
kama vile umeme, maji pamoja na nishati mbadala ili kuwapunguzia wanawake mzigo
wa majukumu mengi katika maeneo ya vijijini na baadhi ya mjini.
Aidha amesema serikali
itaongeza upatikanaji wa teknolojia rahisi na sahihi ili kuongeza tija na
ufanisi katika shughuli zinzazofanywa na wanawake katika uzalishali mali.
Makamu wa Rais amesema hatua
nyingine ni pamoja na kuongeza fursa za elimu kwa wanawake ikiwemo kuanzisha
shule za sayansi kwa wasichana, elimuya ufundi stadiili kuwapatia ujuzi na
stadi zinazowezesha kuzalisha kwa tija.
Hatua nyingine ni pamoja na kuwawezesha
wanawake kumudu na kutumia teknolojia za kidijitali kwaajili ya kuongeza
ushindani katika uzalishaji na shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Kuwawezesha wanawake kupata
afua za kifedha kwa kutumia ubunifu wa aina mbalimbali ikiwemo kutumia njia za
kielektroniki.
Kuondoa fikra na tamaduni
potofu zinazozuia wanawake kujihusisha na shughuli za kiuchumi ikiwemo umiliki
wa ardhi.
Kupanua wigo wa huduma za
hifadhi ya jamii ili kujumuisha kaya ambazo zipo nje ya uchumi rasmi.
Urasimishaji wa biashara
zenye staha zinazofanywa na wanawake ili kuweza kupata huduma za kifedha.
Kuimaraisha mifuko ya
uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kurahisisha kupata mitaji ya kuanzisha
shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mara
baada ya kuwasilisha ahadi hizo, Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo
na Dkt.
Phumzile Mlambo Ngcuka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia masuala ya wanawake (Un- Women)
Dkt Phumzile amesema amefurahishwa
na ahadi zilizotolewa na serikali ya Tanzania katika kuchagiza haki za kiuchumi
za wanawake na kumpongeza makamu wa Rais kwa uwakilishi mzuri. Makamu wa Rais amemuhakikishia Dkt Phumzile
kwamba Tanzania itaendelea kusimamia na kulinda haki za kiuchumi za wanawake.
No comments:
Post a Comment