Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amewaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Tanzania na wa Afrika Mashariki kabla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara za SMZ katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, aliowateua hivi karibuni na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi mbali mbali aliowateuwa  Julai 10, 2021 kushika nyadhifa tofauti katika Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Dk. Mwinyi amemuapisha Mussa Haji Ali kuwa Katibu Mkuu (OR), Ikulu pamoja na  Issa Mahafoudh Haji kuwa Katibu Mkuu (OR) Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

Wengine ni  Dk. Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu (OR) Kazi, Uchumi na Uwekezaji na Mikidadi Mbarouk Mzee kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR)  Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Aidha, amemuapisha Aboud Hassan Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR) Fedha na Mipango anaeshughulikia Fedha na Mipango.

Miongoni  mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na  Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdalla , Jaji Mkuu wa Zanzibar

Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Said Haji, Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Kitwana Idrisa Mustafa, Mawaziri, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na  Usalama pamoja na wanafamilia.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.