Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar,Rukia Mtingwa akifurahia jambo na mgunduzi wa teknolojia, Said Sugu wakati wa uzinduzi wa Kijiji cha kidigitali ‘Digital Village’ ambacho ni maalumu kwaajili ya watu kujifunza matumizi ya mtandao wa 4G. Kulia ni Soud Hassan, mbunifu wa teknolojia.Wagundunduzi hao wamefanikisha kutengeneza vitu mbalimbali ikiwamo helikopta na magari wakitumia kipaji na intaneti kama nyenzo ya kujifunzia.
·
Watu kujifunza namna ya kujiendeleza kielimu na kuendesha biashara
mtandaoni
Zanzibar.
Kampuni ya simu ya ZANTEL imezindua kijiji
cha kidigitali, eneo ambalo limewekwa miundombinu imara ya intaneti kwa
lengo la kutoa mafunzo kwa wakazi wa Zanzibar namna bora ya kutumia mitandao
katika kujiendeleza kielimu na kibiashara.
Hatua hii ni miongoni mwa utekelezaji wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki
Zantel 4G’ awamu ya pili, ambayo pamoja na mambo mengine ina lenga kutoa elimu
kwa wakazi wa Zanzibar juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo
ya kijamii na uchumi.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Zantel wa kuchochea mageuzi ya
kimtandao na kufanya watu waishi kidigitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa
Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema kuwa kituo hicho cha Kiditali kitatoa
huduma za kimtandao bure kwa wakazi wa Zanzibar ndani ya miezi miwili.
“Sehemu hii ina wataalamu na wabobezi
wa huduma hizo za Elimu na Biashara za mtandaoni ambao watakuwa wakitoa mafunzo
kwa watu watakaofika hapa, namna ya kutumia mtandao wa 4G kupata huduma hizo,” alisema.
“Elimu ya mtandaoni si kwa ajili
ya wanafunzi wa shule na vyuo tu, bali hata kwa watu wenye vipaji mbalimbali na
wafanya biashara wanaweza kujifunza kupitia mtandao namna bora ya kukuza na
kutangaza kazi zao na kuboresha. Kwa mfano leo hii tuko na Said Sugu ambaye yeye ameweza
kutengeneza magari, helikopta kwa kutumia kipaji chake na mtandao kuongeza
ujuzi,” alisema
Wafanya biashara pia wana fursa
ya kupata masoko mapya mtandaoni. Wakiwa hapa katika kijiji
cha kidigitali,
watafundishwa namna rahisi ya kutumia mitandao kuuza na kutangaza biashara zao.
Pamoja na hilo, Zantel imezindua shindano la
kidigitali ambalo linatoa fursa kwa watu mbalimbali kuonesha vitu ambavyo
wamejifunza na kutengeneza kwa kutumia mtandao na kujishindia zawadi hadi
Sh300,000.
“Unachotakiwa kufanya ni kutengeneza video fupi na
kuipost kwenye mtandao wa kijamii na kutag kurasa za Zantel.Video ambayo
itapendwa zaidi itajishindia zawadi hadi Shilingi 300,000,” alisema.
No comments:
Post a Comment