Wazri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mh.Selemani Jafo akitaka ufafanuzi zaidi juu ya changamoto za kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Azam kutoka kwa Mkuu wa Viwango vya Bidhaa katika kiwanda hicho Tumaini Fredrik, wakati wa Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwandani hapo nakumalizikia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL 3.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na
Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano
wakisikiliza maelezo kuhusu kiwanda cha Azam na Mji wa Fumba kutoka kwa
Mtendaji katika Kiwanda hicho (hakupatikan jina) wakati wa Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya
Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar
(SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwandani hapo
nakumalizikia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL 3.
Waziri
wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma
Kassim ali akijibu hoja zinazohusiana na jengo la abiria TERMINAL 3 wakati
wa Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja
ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar
(SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwanda kinachozalisha
maziwa cha Azam Fumba nakumalizikia katika Uwanja wa Ndege
wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Wazri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mh.Selemani Jafo
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ya muungano mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya
Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar
(SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwanda kinachozalisha
maziwa cha Azam Fumba nakumalizikia Uwanjawa ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL
3.
Waziri wa Feadha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akitolea Ufafanuzi masuala ya fedha kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwanda kinachozalisha maziwa cha Azam Fumba nakumalizikia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL 3. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Issa
Mzee - Maelezo
Waziri
wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Suleiman Jafo amesema hoja mbalimbali za
muungano zinaendelea kushughulikiwa na kamati ya pamoja ili kuhakikisha zinapatiwa
ufumbuzi wa kudumu.
Akizungumza
mara baada ya ziara ya wajumbe wa kamati ya pamoja walipotembelea kiwanda cha Maziwa
Fumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la (Terminal
III).
Amesema miradi hiyo ya kimkakati ni miongoni
mwa hoja za Muungano ambazo zinatafutiwa ufumbuzi na kamati ya pamoja ili
kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa lengo la kuimarisha umoja uliopo.
Aliwataka
wananchi wafahamu kuwa serikali zote mbili bado zinaendelea kukaa pamoja na
kujadili hoja mbalimbali za muungano kwa maslahi ya wananchi.
Nae
waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mwigulu Nchemba amesema tayari hoja mbalimbali katika masuala ya fedha
zimepatiwa fumbuzi ikiwemo suala la fedha kutoka uhamiaji
na kodi ya ongezeko la thamani.
Alieleza kuwa ulipaji wa kodi upande mmoja unamuwezesha
mwananchi kupata unafuu na kurahisisha mzunguko wa biashara nchini.
Alisema
juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Zanzibar katika kuimarisha
Viwaja vya Ndege ni muhimu kwa maendeleo kwani majengo ya kisasa yanasaidia
katika kuimarisha sekta ya utalii nchini.
Aliwataka
wanachi kuendelea kushirikiana na
viongozi wao katika kutunza miundombinu ili waweze kuimarisha zaidi viwanja vya
ndege kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment