Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari hii leo Vuga - Zanzibar kuelezea Vikao vya Muungano ngazi ya Mawaziri wa SMT na SMZ na kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ, ambacho Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vinaanza kesho tarehe 23/08/2021 Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Saada Mkuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Saada Mkuya wakiongea na waandishi wa habari hii leo Vuga – Zanzibar. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit Faina na Bw. Khalid Amran Mratibu Mkuu wa Shughuli za SMZ –Dodoma.
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hii leo Vuga - Zanzibar kuelezea vikao vya kushughulikia masuala ya Muungano vitakavofanyika Zanzibar tarehe 23-24 Agosti 2021. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari hii leo Vuga - Zanzibar kuelezea vikao vya kushughulikia
masuala ya Muungano vitakavyofanyika Zanzibar tarehe 23-24 Agosti 2021.
Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Selemani
Jafo amesema tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kushughulikia hoja za Muungano
kupitia vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ mwaka 2006, hoja 25
zimejadiliwa na mpaka sasa hoja saba (7) zimepatiwa ufumbuzi na hoja kumi na
nane (18) zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Waziri Jafo ameyasema hayo hii leo Zanzibar wakati akizungumza
na Waandishi wa habari kuelezea kuanza kwa vikao ngazi ya Mawaziri na Kikao cha
Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ kitakachofanyika kuanzia tarehe 24/08/2021
katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul – Wakil, Kikwajuni chini ya Uenyekiti wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimeweka utaratibu wa kutatua
changamoto za Muungano kupitia mfumo rasmi wa Vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT
na SMZ ya kushughulikia Masuala ya Muungano” Jafo alisisitiza.
Amesema kuwa baada ya kikao cha Mawaziri wa SMT na
SMZ, wajumbe watapata fursa ya kutembelea miradi ya kimkakati ya Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal III) na kiwanda cha Maziwa
cha Bakhresa ambayo ni miongoni mwa hoja za Muungano ambazo zimekuwa
zikitafutiwa ufumbuzi na
Vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ hufanyika katika
ngazi tatu ambazo ni:- Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ, Mawaziri wa SMT na SMZ na
kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ, ambacho Mwenyekiti wake ni Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo la kuweka utaratibu huu ni
kuimarisha Muungano kwa kuhakikisha changamoto zote zinatafutiwa ufumbuzi wa
kudumu.
No comments:
Post a Comment